Home » » KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD YASHINDA TENA TUZO YA UBORA

KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD YASHINDA TENA TUZO YA UBORA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo akimkabidhi meneja uzalishaji wa kampuni ya  Asas Dairies Ltd Bw Lipita  Mtimila tuzo baada ya  kampuni yake  kushinda  tuzo ya  ubora katika maonyesho ya  wiki ya Maziwa Nchini
Tuzo  ya  Ushindi  ya mwaka 2016
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo akitembelea  banda  la kampuni ya  Asas dairies Ltd
Viongozi  wakitazama bidhaa za  kampuni ya  Asas
Wanafunzi  wakiwa katika  picha ya  pamoja  katika  maonyesho ya   wiki ya Maziwa
Meneja  uzalishaji  wa kampuni ya  Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila akionyesha cheti  cha  ushindi wa jumla  ambacho kampuni   hiyo  ilikabidhiwa
Bw  Mtimila akionyesha  vyeti  vya  ushindi wa  uzalishaji  wa bidhaa bora
Vyeti vya  ushindi 
                            Na Matukiodaima Blog                  

KAMPUNI  ya Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea kushika nafasi ya  kwanza kitaifa   uzalishaji wa maziwa nchini . 

Kampuni  hiyo imeshinda tuzo  ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora  za maziwa  katika mashindano   wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya  shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe .

Kampuni  hiyo imeibuka  mshindi  wa  kwanza  baada ya  kuongoza  katika nafasi zote  tatu  za  ubora  wa  bidhaa zilizoshindanishwa  katika mashindano  hayo .

Akikabidhi tuzo hizo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo pamoja na kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza  kampuni   ya Asas Dairies  Ltd  kwa   kufanya  vizuri katika mashindano hayo ya ubora  wa maziwa nchini 
Alisema  kuwa jitihada  zilizoonyeshwa na kampuni  hiyo ni kubwa na  zinapaswa  kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.

Kwani  alisema  kuwa  kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa si  jambo dogo ni  jitihada  kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.


Pia     aliipongeza  bodi ya maziwa Tanzania kwa  kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya  kipimo kwa  wamiliki wa  viwanda vya maziwa  nchini na sehemu  ya  kujitathimini  .


Kwa upande  wake  meneja  uzalishaji  wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd  Lipita Mtimila   alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu bado  ilipata  kuongoza katika mashinadano kama haya  miaka  mitatu  nyuma  na  hii ni mara ya nne  kuongoza .

Katika mashindano hayo  yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa  Tanzania( TDB)  kampuni ya Asas Dairies iliweza  kuibuka na ushindi  wa  jumla baada ya kushinda tuzo zote  tatu  dhidi ya makapuni  mengine  ya uzalishaji maziwa  yaliyoshiriki katika mashindano hayo .

Bw Mtimila aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd  na  kuwa  lengo la kampuni  hiyo ni kuendelea  kuzalishaji bidhaa zenye  ubora zaidi .

Pia  alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaoutoa kwa  kuendelea  kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa
KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD YASHINDA TENA TUZO YA UBORA Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo akimkabidhi meneja uzalishaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila tuzo baada ya kampuni yake kushinda tuzo ya ubora katika maonyesho ya wiki ya Maziwa Nchini Tuzo ya Ushindi ya mwaka 2016 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo akitembelea banda la kampuni ya Asas dairies Ltd Viongozi wakitazama bidhaa za kampuni ya Asas Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja katika maonyesho ya wiki ya Maziwa Meneja uzalishaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila akionyesha cheti cha ushindi wa jumla ambacho kampuni hiyo ilikabidhiwa Bw Mtimila akionyesha vyeti vya ushindi wa uzalishaji wa bidhaa bora Vyeti vya ushindi Na Matukiodaima Blog KAMPUNI ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa uzalishaji wa maziwa nchini . Kampuni hiyo imeshinda tuzo ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora za maziwa katika mashindano wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe . Kampuni hiyo imeibuka mshindi wa kwanza baada ya kuongoza katika nafasi zote tatu za ubora wa bidhaa zilizoshindanishwa katika mashindano hayo . Akikabidhi tuzo hizo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo pamoja na kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza kampuni ya Asas Dairies Ltd kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa nchini Alisema kuwa jitihada zilizoonyeshwa na kampuni hiyo ni kubwa na zinapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini. Kwani alisema kuwa kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa si jambo dogo ni jitihada kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo. Pia aliipongeza bodi ya maziwa Tanzania kwa kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya kipimo kwa wamiliki wa viwanda vya maziwa nchini na sehemu ya kujitathimini . Kwa upande wake meneja uzalishaji wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Lipita Mtimila alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu bado ilipata kuongoza katika mashinadano kama haya miaka mitatu nyuma na hii ni mara ya nne kuongoza . Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa Tanzania( TDB) kampuni ya Asas Dairies iliweza kuibuka na ushindi wa jumla baada ya kushinda tuzo zote tatu dhidi ya makapuni mengine ya uzalishaji maziwa yaliyoshiriki katika mashindano hayo . Bw Mtimila aliwataka watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd na kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuendelea kuzalishaji bidhaa zenye ubora zaidi . Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa kuendelea kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa