Home » » WANAOLIMA KWENYE MAENEO OEVU WAONDOKE- RC MASENZA

WANAOLIMA KWENYE MAENEO OEVU WAONDOKE- RC MASENZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda  akitangaza  washindi wa  tuzo  za uhifadhi  mazingira za TANAPA 
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kulia na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  wakimpongeza mwakilishi wa  kikundi cha familia ya Festo  Mhanga  wa Kilolo  kwa  kushinda  tuzo ya Mazingira ya  Tanapa na  kuzawadiwa shilingi  milioni  jana  wakati wa kilele  cha  siku ya Mazingira na utoaji wa Tuzo za TANAPA kwa  wananchi wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya 
Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira  duniani jana  Amos Makala  mkuu wa  mkoa wa Mbeya  akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  na meneja  ujirani mwema wa Tanapa Ahmed Mbugi  kushoto 
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akitoa  salam siku ya  Mazingira  Duniani mkoani  Mbeya 
Kikundi  cha  skauti cha elimisha jamii  wilaya ya  Mufindi wakikabidhiwa  hundi ya shilingi  milioni 1 toka Tanapa 
Mkuu  wa  mkoa wa Njombe Christopher  Ole Sendeka  akitoa  salam  siku ya mazingira  duania
Na  matukiodaimaBlog  
SERIKALI Imewataka wananchi wanaolima kilimo   kwenye maeneo oevu maarufu kama vinyungu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya nje ya kilimo  hicho  kulinda mto  Ruaha mkuu kukauka.

Akitoa salam  za mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya  tuzo ya TANAPA ya uhifadhi mazingira na kilele cha siku ya  mazingira Duniani leo maadhimisho yaliyofanyika kwa kijiji cha Madabaga wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Jana mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema iwapo ulimaji wa vinyungu utafumbiwa macho mto  Ruaha mkuu utaendelea kukauka.

Alisema kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya mto  Ruaha mkuu  pamoja na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Kwani alisema uhifadhi wa hifadhi ya Ruaha ni pamoja na uhifadhi wa mto  Ruaha mkuu hivyo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wana wajibu wa kulinda mto  Ruaha mkuu na kuchukua hatua kwa wote wanaolima kwenye vy
Wakuu  wa wilaya ya Mbeya na Mufindi  wakijadili  jambo 
Mgeni  rasmi  katika  kilele  cha siku ya mazingira  duania Amos Makala  mkuu wa mkoa wa Mbeya  na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi  wengine  wakiwasilia  uwanja wa maadhimisho ya siku ya mazingira  duniani 
anzo vya maji na chini ya mita 60 kutoka  kingo za mito .

Masenza alisema wajibu wa kulinda mto  Ruaha mkuu upo mikononi mwa viongozi wote wakianza wale wa serikali za vijiji.

" Niwaombe sana wananchi wote tuungane kulinda mto  Ruaha na jambo hili uwe ni utamaduni wetu na halihitaji suluti "

Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda alisema kwa siku ya mazingira ambayo ni mwaka wa pili kufanyika mikoa ya Njombe,Mbeya na Iringa huambatana na tuzo kwa vikundi na mtu  mmoja mmoja anayefanya vema katika uhifadhi.

Alisema kwa mwaka jana  ndipo zoezi la utoaji tuzo lilianzishwa kwa kuwa na washiriki 200 ila  idadi ya washiriki kwa mwaka huu imeingezeka hadi kufikia washiriki zaidi ya 500.

Maronda alisema kuwa uharibifu wa ikolojia ya mto  Ruaha mkuu umeendelea kuharibiwa na urejeshaji wa mto  unaoharibiwa gharama yake  ni kubwa zaidi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala alisema kimataifa maadhimisho hayo yamefanyika nchini Canada na kitaifa yamefanyika mkoani Mara.

Hivyo alisema maendeleo ya uchumi wa nchi uende sambamba na uhifadhi wa mazingira na kuwa suala la uchomaji ovyo pamoja na kilimo kisichoendelevu hakitavumilika.

Alisema tayari makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kunusuru ikolojia ya mto  Ruaha mkuu hivyo viongozi wote wanapaswa kusimamia Sheria zilizopo na kuepuka siasa zinazochangia uharibifu wa mazingira.

" Hivyo nawaomba sana viongozi na wananchi wote kusimamia sheria kwa kutoa elimu na kazi ya kusimamia sheria inatupaswa tuifanye sisi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya maana sisi hatupigiwi kura.

Hivyo alisema njia pekee ya kulinda mazingira ni kupanda miti kwa kila wilaya miti milioni 1.5 na kwa kila mkoa miti milioni 15.


Kuhusu mifugo kuongezeka alitaka senza ya mifugo kufanyika na baada ya hapo ng,ombe  zote zitapigwa chapa kuitambua na mifugo iliyopo katika hifadhi kama Ihefu kuondolewa haraka.

Mwisho


0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa