Home » » FILIKUNJOMBE APELEKEWA FOMU YA UBUNGE NYUMBANI KWAKE , MWENYEWE AMPONGEZA JK ASEMA DR MAGUFULI ATEGEMEE KURA ZA KISHINDO LUDEWA‏

FILIKUNJOMBE APELEKEWA FOMU YA UBUNGE NYUMBANI KWAKE , MWENYEWE AMPONGEZA JK ASEMA DR MAGUFULI ATEGEMEE KURA ZA KISHINDO LUDEWA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipokea  fomu  kutoka kwa  wazee  na vijana  waliomchukulia na kwenda  kumkabidhi nyumbani kwake Ibani mjini  Ludewa jana
Msafara  wa  vijana wa Boda  boda  zaidi ya 300  waliowasindikiza  wazee wa Ludewa kumchukulia  fomu  mbunge  Deo Filikunjombe
Wazee  wakimpoelekea  fomu ya ubunge Deo Filikunjombe nyumbani kwake  kwa maandamano
Safari  ya  kuelekea  nyumbani kwa Filikunjombe kukabidhi fomu ya ubunge
Wazee  hao  wakiwa nyumbani kwa mbunge  Filikunjombe kumkabidhi  fomu ya ubunge Ludewa
Hapa  wakimkabidhi fomu Bw  Filikunjombe

Askari wa usalama barabarani  akiongoza usalama
Filikunjombe  akielekea  kuwashukuru  wananchi Ludewa kwa  kumchukulia  fomu ya  ubunge
Ni zaidi ya  furaha kwa mbunge  Filikunjombe
Kikundi  cha Mganda
Wananchi wakimsikiliza mbunge  wao Filikunjombe
Wawakilishi  wa wananchi wa jimbo jirani la spika  Makinda  wakimpongeza Filikunjombe
Filikunjombe  akiwa amepokea  zawadi ya mikuki kama  zawadi kutoka kwa wananchi wa  jimbo la Makinda ambao  walifika  kumpongeza  pia
Hapa  akikabidhiwa
Filikunjombe  akiwashukuru kwa  moyo wa upendo
Mkazi wa Ludewa akionyesha  furaha yake kwa mbunge
Wadau mbali mbali  wakimchangia  pesa  ya fomu Filikunjombe
Filikunjombe  akikabidhiwa  pesa  za kampeni  na fomu
Wananchi  wakifurahia  kuonyesha  imani  tena na Filikunjombe
Filikunjombe  akizungumza na wananchi hao
Hotuba ya kipindi cha  miaka mitano madarakani
Filikunjombe na familia  yake  wakifurahia upendo wa wana Ludewa
 Na  MatukiodaimaBLog
WAZEE Ludewa  waamchukulia  fomu Deo Filikunjombe wakimwomba  kuendelea kuongoza  jimbo  hilo kwa miaka 20  zaidi huku wakidai kuwa kama  usingekuwa ni utaratibu  wa  chama  cha mapinduzi (CCM) na  ule wa  tume ya uchaguzi (NEC)  wa  kufanya uchaguzi kila  baada ya miaka  mitano basi  wao wangempitisha mbunge  huyo bila kupingwa na uchaguzi kwa wilaya ya Ludewa ungekuwa wa madiwani pekee na sio kwa mbunge urais Dr John Magufuli  wala mbunge  wao  huyo .

Mwenyewe awaunga  mkono asema anajivunia  uchapakazi wa Rais Dr  Jakaya  Kikwete kwani ni Rais pekee  aliyesaidia  kuiwezesha  Ludewa kusonga  mbele na  kuwa  zawadi ambayo wananchi wa Ludewa  wanaitoa kwa CCM ni  kuhakikisha mgombea  urais wa CCM Dr Magufuli anapata  kura  nyingi  zaidi  ukilinganisha na wilaya yoyote  hapa  nchini kwani pia amehusika kuwakomboa wananchi wa Ludewa kwa kutengeneza barabara  za  wilaya   hiyo.

Wakizungumza    wakati  wa kumkabidhi   fomu   nyumbani  kwake  Ibani mjini  Ludewa   wazee hao  walisema  wamelazimika  kumchukulia  fomu hiyo na  kwenda  kumkabidhi  baada ya  kuridhishwa na  kazi kubwa  aliyoifanya kwa  kipindi  cha miaka mitano ambayo amepata  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo na  kuonyesha  utendaji  mkubwa zaidi  ukilinganisha  namaendeleo yaliyoonyeshwa na  wabunge 7 waliotangulia  katika   jimbo  hilo .

Hivyo  walisema bado wanaimani  kubwa na  mbunge  wao na  kuwa imani na matumaini ya  wananchi wa  Ludewa ni kuona  Filikunjombe anaendelea  kuwatumikia  wananchi hao  kwa  vipindi vingine  4 kwa maana ya  miaka 20 ama  kuendelea  kuongoza  jimbo  hilo hadi pale atakapoamua   kustaafu mwenyewe  kwani utendaji kazi  wake  wa kazi ndio ambao  umemfanya kupewa dhamana   hiyo ya kuendelea   kuongoza jimbo  hilo.

" Tumekuamini na  tumependezwa na utendaji kazi  wako   hivyo wewe  tunakubariki kuendelea  kuongoza  tena na tena  jimbo  hilo kwani  ulipokea  likiwa katika hali mbaya na  sasa wananchi wa Ludewa  kupitia  jopo  la wazee  tumekuamini  zaidi na tumekuchukulia  fomu  hii ya ubunge kama  ishara ya  kukuamini  zaidi ......tulikuita jembe na  sasa  wewe ni katapila letu  Ludewa umeweza kupita  pasipo pitika  umetufanikishia maendeleo makubwa kwa  kipindi  kifupi  zaidi "

Kwa  upande  wake  mbunge  Filikunjombe pamoja na  kuwashukuru wazee hao  na  vijana  wa boda  boda  zaidi ya 300 katika  wilaya ya  Ludewa  walioungana kumchukulia  fomu  hiyo  alisema kuwa imani  kubwa na ushirikiano mkubwa ambao  wananchi wa Ludewa  wameuonyesha  wakati wa utumishi  wake umemfariji na kuweza  kufanya kazi kubwa  zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatumikia  vema  buneni  pasipo kusinzia kama  walivyofanywa baadhi ya  wabunge  wengine.

Filikunjombe  alisema  ili kuwa ni  vigumu kwake kusinzia bungeni kutokana na aina ya makubaliano yake na  wananchi  waliomtuma kwenda  kuwawakilisha na kuwa wananchi hao  walimtuma kuwasemea bungeni  hivyo kama nae angeungana na baadhi ya  wabunge ambao  uwakilishi wao bungeni  ulikuwa ni kusinzia basi wilaya ya Ludewa isingekuwa na maendeleo  kiasi hicho.

Alisema  kuwa  leo hata  wale wananchi wa Ludewa ambao  walikuwa  wakikwepa kuitwa  wana Ludewa  kutokana na uduni wa maendeleo  uliokuwepo katika wilaya  hiyo  hivi  sasa  wameanza  kutembea  kifua mbele  kujivunia  wilaya  yao tofauti na  zamani ambapo  wengi  wao  walikuwa  wakidanganya  kuwa  wanatoka  mkoa  wa Ruvuma.

" Kazi  mlionituma  bungeni  Dodoma  nimeifanya zaidi  ya uwezo  wangu na ndio maana  leo  wilaya  yetu  imepiga hatua  kubwa katika maendeleo na ukweli nimefanya  yale  mlionituma  bungeni ombi langu kubwa  kwenu  wenzangu naomba mzidi  kuniombea afya njema  zaidi na  kuniunga mkoni  ili nikirudi bungeni tena  kuweza  kufanya mengine makubwa  zaidi ya haya"

Alisema  kuwa  hawezi  kusema wabunge  waliotangulia hawakufanya  chochote kabisa katika jimbo la Ludewa japo  kila mmoja aliweza kufanya kulingana na uwezo  wake ikiwa ni pamoja na mbunge wa kwanza kuleta  meli ,mbunge mwingine  alileta basi ,mwingine  umeme Ludewa mjini lakini kwa upande wake amefanya  zaidi  ya hayo na  kuifanya  wilaya  hiyo kuwa  wilaya  ya mfano katika  wilaya za  mkoa wa Njombe huku akisisitiza  kuwa lengo yake ni kuona  wilaya ya Ludewa  inaendelea  kuongoza kwa maendeleo  ukilinganisha na  wilaya  zote za  mkoa  wa Njombe.

Kwani alisena nia, uwezo na nguvu ya  kuifanya wilaya  ya  Ludewa  kuongoza katika maendeleo bado anayo na  kuwa kazi kubwa ya  wananchi  wa Ludewa  kuendelea  kutoa ushirikiano kwake tena .

Hata   hivyo  alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika wilaya  hiyo kamwe hataacha  kumpongeza Rais Dr Kikwete ambae  amekuwa sehemu ya mafanikio  yake na  mafanikio ya  wananchi  wa Ludewa katika maendeleo ila  pia  aliyekuwa  waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambae  saa ndie Rais mtarajiwa wa awamu ya  tano  kwani kati ya  mawaziri  waliopambana kwa ajili ya Ludewa Dr Magufuli ni namba moja na kuwa  zawadi yake ni  kupata  kura za  kishindo katika wilaya  hiyo ya  Ludewa .

Alisema  Rais Dr  Kikwete kwa upande  wake tayari amekwisha ahadi kufika kuwaaga  wananchi wa Ludewa kabla ya  kumaliza  muda  wake kwa  kuzindua  ujenzi wa  viwanda  vya  chuma katika wilaya   hiyo ila pia Dr Magufuli  anataraji  kufika katika  wilaya  hiyo ya  Ludewa wakati  wowote  kuanzia  sasa  hivyo pamoja na  kuwashukuru  viongozi hao  wakubwa kwa upendo  wao kwa wana Ludewa  bado alisema historia kubwa  wameiandika katika wilaya   hiyo.

Katika zoezi  hilo la wazee  kumkabidhi fomu ya  ubunge  Bw  Filikunjombe  zaidi ya Tsh 400,000 zikichangwa na wananchi  mbali mbali yakiwemo makanisa na  watu  binafsi pamoja na mbuzi na zawadi nyingine kama  sehemu ya  kumuunga mkono mbunge  huyo katika  safari yake ya  kugombea tena  ubunge wa  jimbo  hilo la Ludewa

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa