Wakazi
wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa wakiwa na hati zao za
umiliki wa ardhi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi (aliyevaa miwani)
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani
(USAID) Ndugu David Thompson na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya hati miliki za ardhi zikiwa zinaandaliwa ili kugawiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Ndugu
Yohanes Keng’ena na Mkewe Elizabeth Makang’olo wakipokea hati miliki ya
ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa William Lukuvi.
Bibi
Catherine Abdallah akipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Ndugu
Petro Wilson na Mkewe Leila Mlawa wakipokea hati miliki ya ardhi kutoka
kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William
Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
akiongoza ukataji utepe katika ufunguzi wa masijala ya ardhi ya kijiji
cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Mkurugenzi
wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Ndugu David Thompson
akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Moja ya shamba la mkazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
amewakabidhi hati miliki 810 za ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha
Kinywang’anga kilichipo Mkoani Iringa.
Wananchi
hawa wamekabidhiwa hati hizo za umiliki wa ardhi baada ya kupimiwa
maeneo yao ya viwanja na mashamba wanayoyamiliki na kuandaliwa hati
miliki ambazo walikabidhiwa na Waziri wa Ardhi Mheshimiwa William Lukuvi
kijijini hapo.
Katika
tukio lingine Mheshimiwa William Lukuvi amezindua masijala ya ardhi ya
kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma ya utoaji
na uhifadhi wa hati miliki za ardhi.
Akizungumza
na wakazi wa Kijiji hicho mara baada ya kuwakabidhi hati miliki zao za
ardhi na kuzindua baraza hilo Waziri Lukuvi aliwasihi wananchi hao
kuzihifadhi na kuzitunza hati zao hizo ili kuepukana na migogoro ya
ardhi inayowakabili wananchi wengi wasio na hati miliki nchini.
Nae
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID)
walioshirikiana na Serikali kuwezesha uandaaji wa hati miliki hizo Ndugu
David Thompson amemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuja na kuwakabidhi Wananchi hati
hizo na kuwaombaa Wananchi kuzitumia kwa maendeleo yao.
Wananchi
wa Kijiji cha Kinywang’anga wamemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi pamoja na shirika la USAID
linaloendesha mradi wa ‘Tanzania Land Tenure Assistance’ kwa
kuwaaezesha kupata hati hizo maana ilikuwa kero kubwa katika kata yao.
Aidha,
Waziri wa Ardhi ametoa hati miliki hizo ili kutekeleza Programu ya
Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi yenye
lengo la kutekelezwa nchi nzima. Utekelezaji huu utahusisha kuhakiki
mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo mengine yote nchini na kupima
kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa
wananchi, taasisi na Kampuni.
Sambamba
na hilo, Matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa,
Wilaya, Hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya
mipaka yote nchini kuhakikiwa na kukamilika.
Aidha
mpango huu unalenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika
kupanga, kupima, na kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za
vipande vya ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya
ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Serikali
ya awamu ya tano imeweka adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo
sasa na kuzuia kasi ongezeko la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano
kwa kuandaa mpango kabambe wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa
kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na
mashamba.
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)
0 comments:
Post a Comment