Na Francis Godwin, Irina
MOTO mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza tena bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Wiliam Lukuvi pawaga wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizio jana mkuu wa shule hiyo Charles Mgimwa alisema kuwa moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 5.30 asubuhi ya jana wakati wanafunzi wakati wanafunzi wote wakiwa darasani wakiendelea na vipindi na ndipo waliposhuhudia moto ukiwakati katika bweni hilo baada ya kuona moshi mwingi angani .
Alisema kuwa bweni hilo linalikuwa likitumiwa na wanafunzi 64 wavulana na kuwa hadi sasa hawajui chanzo cha moto huo kwani wakati moto ukitokea umeme haukuwepo toka Tanesco walivyokata umeme majira ya saa 3 asubuhi .
Mkuu huyo alisema uwezekano wa kuzima moto huo ulikuwa ni mdogo kutokana na kuanzia kuwaka katika paa na hivyo kutokana na kutokuwepo kwa gari la zima moto ama vifaa vya kisasa vya kuzimia moto huo uwezekano wa kuokoa mali za wanafunzi ama kuzima moto ulikuwa ni mdogo.
Akielezea kuhusu hasara ambayo imetokea alisema kuwa bado wanaendelea kufanya thathimini ya hasara hiyo japo vitu vyote wanafunzi vikiwemo vitanda na magodoro na nguo zimeteketea na moto huo .
Mgimwa alisema bado hawajajua kuhusu nini kifanyike kama kufunga shule ama hadi hapo atakapopata ruhusa kutoka ngazi ya juu japo kwa sasa wanafunzi hao watawaombea kwa wenzao wanaoishi mitaani ili kujihifadhi .
Afisa mtendaji wa kijiji cha Magozi Shaibu Mwoneka alisema kuwa bado hawajajua chanzo hasa cha moto huo kwani umezuka katika mazingira ya kutatanisha
Hii ni mara ya pili bweni hilo la wavulana katika shule hiyo ya sekondari ya Wiliam Lukuvi kuungua moto mara ya kwanza liliungua moto mwaka juzi
MWISHO
0 comments:
Post a Comment