Home » » UCHAGUZI KILOLO KURUDIWA KESHO‏

UCHAGUZI KILOLO KURUDIWA KESHO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

NA RAYMOND MINJA IRINGA
 
 
MOTO wa kisiasa umeendelea kulipuka katika jimbo la Kilolo mkoani
Iringa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kilolo anayemaliza muda wake,
Profesa Peter Msolla kushinda  rufaa iliyokuwaikipinga matokeo
yaliyompa ushindi Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Tabora, Venance Mwamotto
katika kura za maoni za ubunge za Chama cha Mapinduzi (CCM) jimboni
humo.
 
 
Hii itakuwa ni mara ya pili kurudiwa kwa uchaguzi huo kwani apo awali
kata tatu kati ya kata 24 zilirudia upya kupiga kura kwa kile
kilichodaiwa makatibu kumuongezea kura profesa Msolla na uchaguzi
uliporudiwa Venance Mwamoto alikuwa mshindi wa kwanza kwa kupata kura
11,200, Profesa Msolla  alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 10,014
katika uchaguzi huo ulioshirikisha jumla ya wagombea 15.
 
 
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kilolo, Clement Mponzi alisema watarudia
uchaguzi katika kata 27 kwa ngazi ya ubunge kwa madai kuwa kuna
mgombea hakuridhika na matokeo hivyo ili kumaliza utata na kila mtu
kuridhika na matokeo inabidi uchaguzi huo kurudiwa
 
 
Mponzi alisema uchaguzi huo utakao rudiwa kesho October 12 kuanzia
majira ya saa mbili asubuhina kumalizika saa kumi jioni  huku
akiwataka wagombea kuwawahisha mawakala wao mapema katika vituo vya
kupigia kura ili kuepuka lawama zisizo kuwa na msingi
 
 
Hapo awali kabla Profesa Msolla hajaenda kukata rufaa  alisema kabla
ya matokeo hayo kutangazwa bila kuridhiwa na wagombea wote alikuwa
akiongoza kwa kura 13,409 dhidi ya kura 9,749 alizopata Mwamotto.
 
 
Alisema kura zake ziliyoyoma baada ya Katibu huyo  wa wilaya kuamuru
kata tatu za Lugalo, Uhambingeto na Nyalumbu ambazo ni kati ya kata 24
za jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka kumi kutakiwa kurudia uchaguzi
bila kushirikisha kamati ya siasa ya wilaya hiyo kwa madai kwamba
wasimamizi wa uchaguzi wa kata hizo walichelewa kuwasilisha matokeo
yake ndani ya muda uliopangwa.
 
 
“Na kimsingi kata zilizoamuriwa zirudie uchaguzi kwa kisingizio kwamba
matokeo yake yalichelewa wakati kuna kata nyingine nyingi tu nazo
zilichelewesha matokeo yake ni baadhi ya kata ambazo mimi nilipata
kura nyingi zaidi ikilinganishwa na wagombea wengine,” alisema.
 
 
Mgombea anayelalamikiwa kupata ushindi huo kinyemela alisema;
“tulalamika baada ya kuona fomu za matokeo katika kata hizo tatu zina
utata. Malalamiko yetu yalikuwa ya msingi na uchaguzi ukarudiwa na
baada ya kurudiwa matokeo ya jumla yamenipa ushindi”
 
 
Akizungumzia dosari iliyopelekea uchaguzi katika jimbo hilo kurudiwa,
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema kuwa kuna badhi
ya wagombea hawakuridhika na matoke hivyo kwa mujibu wa kanuni na
taratibu za chama hicho wameamuru uchaguzi huo kurudiwa ili kila mmoja
kupata haki yake anayostahili
    

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa