Home » » HOT NEWS: Prof Msola akubali yaishe kwa Mwamoto Kilolo‏

HOT NEWS: Prof Msola akubali yaishe kwa Mwamoto Kilolo‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Matukiodaimablog Kilolo


Mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa Mjini Frederick Mwakalebela ambae ni mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe ( kulia)akimpongezana na Mshindi wa kura za maoni jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ambae ni mkuu wa Wilaya ya Kaliuwa Tabora( picha na MatukiodaimaBlog)

ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Kilolo prof Peter Msolla amekubali kushindwa katika kura za maoni na mkuu wa Wilaya ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw Venance Mwamoto Prof Msolla akiwa mbele ya msimamizi mkuu wa uchaguzi aliyeagizwa na kamati kuu ya CCM Taifa , Luteni mstaafu Christopher Ngaleson na wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya alisema kuwa amekubali kushindwa katika uchaguzi huo na kuyapokea matokeo hayo na kusaini.

katika uchaguzi huo mdogo uliorudiwa jana kwa mara ya tatu sasa na kuwa na baadhi ya kasoro kwa kama ya wananchi wasio katika dadtari la wana Ccm wala Kadi za chama kukutwa wakipiga kura katika kituo cha Mbuyuni kata ya Ruaha mbungeni na kituo cha Msosa wananchi kutumia vitambulisho vya Tume ya Taifa ya uchaguzi wakidai wameambwa na viongozi wao kupiga ili kumwezesha prof Kushinda bado matokeo yalikuwa tofauti kwake.

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi katibu wa CCM wilaya ya Kilolo Bw Clemence Mponzi alisema kuwa wagombea walikuwa 15 katika uchaguzi huo na Mwamoto alishinda kwa kura 13,713 huku akifuata kwa kupata kura 9,810 na nafasi akifuata Danford Mbilinyi aliyepata kura 1,142.

Wakati chelestino Mofuga (576),Thadei Kikoti (136),Merick Luvinga (161),Anosta Nyamoga (68),Yefred Myenza (63),Luciana Mbosa (53),Francis Mkokwa(47),Mgabe Kihongosi (46),Ashraf Chusi (29) na Israel Salufu (9) Kwa upande wake Prof Msolla alisema kuwa amekubali ushindi wa Mwamoto na kuwa yupo tayari kuheshimu maamuzi ya kamati kuu ya Ccm Taifa " Nimekubali matokeo nipo tayari kufanya Kazi na atakayeteuliwa na chama Mimi kwangu chama kwanza mtu baadae" Huku Mgombea Francis Mkokwa mbali ya kumpongeza Mwamoto kwa ushindi huo bado alisema kuwa chama tawala kimeonyesha kumsikiliza Mgombea mmoja ambae alikuwa mbunge japo yeye ndie alicheza rafu katika michakato yote ya kura za maoni kwa kutaka kulazimisha goli la mkono.

Mkokwa alisema idadi ndogo ya wana Ccm ndio walijitokeza kupiga kura kutokana na kuchukizwa na kurudia mara kwa mara zoezi hilo .

Hata hivyo Mkokwa aliwataka viongozi wa Ccm ngazi za juu kuheshimu maamuzi ya wananchi katika kura za maoni kuliko kulazimisha kupita yule wanaemtaka wao kama walivyotaka kufanya katika jimbo hili na wangempitisha prof Msolla ni wazi jimbo hilo lingekwenda upinzani.

Mshindi wa kura hizo za maoni jimbo la Kilolo Bw Mwamoto aliwashukuru wana Ccm kilolo kwa kuonyesha Uwazi wao kwa mara zote uchaguzi uliporudiwa na kuwaomba radhi kwa kurudia uchaguzi huo huku akiwaomba wagombea wenzake kuunganisha nguvu ili kupata ushindi wa kishindo kwa Madiwani ,yeye kama mbunge na Rais Dr John Magufuli

Mwamoto alipata kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo mwaka 2000 hadi 2005 alipo pokeweed jimbo hilo na Prof Msolla ambae ameongeza kwa vipindi viwili sasa.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa