Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya
Kilolo, Gelard Guninita wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya
Wakulima wa Nyanya iliyofanyika katika Kijiji cha Nzih Tarafa ya
Kalenga mkoani hapa.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Muunganisho wa
Ujasilimali Vijijini (Muvi) kwa ushirikiano na wadau wa kilimo kutoka
sekta binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa za taasisi hiyo, zao la
nyanya katika mkoa huo limeongezeka kutoka tani 100,009 mwaka 2010 na
kufikia tani 100,400 kwa kipindi cha mwaka 2013 katika maeneo ambayo
taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Guninita,
ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine
Ishengoma alisema ikiwa wakulima hao wataunda vikundi na kusajili,
watakuwa wametambuliwa na kuwa na sifa za kupata mikopo katika taasisi
za fedha jambo linaloweza kuwasaidia kupata mitaji kwa ajili ya
kuendesha shughuli zao. “Ninaomba mjiunge katika vikundi na sisi
serikalini tunasaidia pale itakapoonekana kuna ulazima,” alisema.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment