Home » » LISHE KWA WATOTO NI DUNI IRINGA

LISHE KWA WATOTO NI DUNI IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
LICHA ya mkoa wa Iringa kuwa ni bakuri na ghara linalotegemewa kwa chakula nchini, bado tatizo la Utapiamlo mkali, unaotokana na lishe duni linawasumbua watoto walio wengi mkoani humo.

Hayo yamezungumzwa na mratibu wa uongezaji wa virutubishi kwenye chakula kutoka jijini Dar es salaam Celestin Mgoba wakati akitoa elimu juu ya umuhimu wa lishe kwa watoto, katika kijiji cha Nzihi na Kalenga Wilayani Iringa.

Mgoba amesema taasisi ya chakula na lishe umeanzisha mpango wa uongezaji wa viinirishe kwenye chakula ngazi ya jamii kwa lengo la kukabiliana na hali ya utapiamlo mkali na udumavu na kuepukana na vifo vitokanavyo na tatizo hilo.

Aidha amesema taasisi ya chakula na Lishe imeanzisha mpango wa uongezaji wa Virutubishi kwenye chakula ngazi ya jamii umewalenga watoto wenye umri wa kuanzi miezi sita hadi miaka mitano, na utazifikia Wilaya sita ya Iringa, Kilolo na Wilaya ya Njombe, Wilaya ya Karatu, Wilaya ya Monduli na Wilaya ya Arumeru.

Naye Martin Chacha afisa lishe Wilaya ya Iringa amesema tatizo la utapiamlo na udumavu katika Wilaya ya Iringa ni asilimia 52 huku asilimia 30 ya watoto hao wakipoteza maisha kwa tatizo hilo.

Chacha amesema katika kukabiliana na hali hiyo, tayari wataalamu na wahudumu mbalimbali wamepatiwa elimu na mafunzo ya umuhimu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula, na kuwa tatizo la utapiamlo na udumavu linatokana na baadhi ya jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya mlo
sahihi wenye vitamin za kutosha.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa