Na Mwandishi Wetu,
Wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilombero wamefanikiwa kupata mkopo wa 890Mn kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga.
Hayo
yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw.
Robert Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa
wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya
Wilaya ya Kilombero.
Bw.
Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350
ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa
utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
“Mkopo
huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika
kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.
Kwa mujibu wa Bw. Paschal mkopo
huo utasaidia shughuli mbalimbali za utayarishaji wa mashamba, kupima
ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa
mpunga pamoja na kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo
mbegu bora, mbolea na madawa.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi
viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo
ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.
“Tunaamini mkopo huu utachagiza kuongezeka
kwa upatikanaji wa chakula na Pato la Taifa kutokana kuongezeka kwa
tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya ongezeko la thamani, ukuaji wa
viwanda vya mazao ya kilimo hivyo kuchangia kuongezeka kwa ajira
nchini,” aliongeza.
Akizungumzia
mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa
mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa
kutumia njia mbalimbali. Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo
mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo;
kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa
mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na
mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa
fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.
“Kwa
kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya
uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo
cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji
kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi
kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye
kuendeleza kilimo,” alisema.
Warsha
hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe
ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha
hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na TADB.
Mhe.
Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na Benki hii
na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali
“Nawasihi
mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze
kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma
kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.
0 comments:
Post a Comment