Home » » KIWANGO CHA UFAULU DARASA LA 7 CHAPANDA WILAYANI MUFINDI

KIWANGO CHA UFAULU DARASA LA 7 CHAPANDA WILAYANI MUFINDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Zaidi ya wanafunzi 5,100 wa shule za msingi Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la 07 ulifanyika mapema mwaka jana, huku ufaulu huo ukipanda na kufikia asilimia 80.39 ukilinganisha na asilimia 68.21 ya mwaka 2014.
 Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya mufindi kwa nyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wanafunzi waliokuwa wamesajiliwa   kufanya mtihani walikuwa 7,220 na miongoni mwao waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni 5,198.
Taarifa hiyo imeainisha mgawavyo wa wanafunzi hao kwa kuzingatia jinsi, ambapo kati ya waliofaulu, wasichana wameongoza kwa takwimu za ufaulu huo wakiwa elfu 2,831 wakifuatiwa na wavulana 2,367. Aidha, wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule ili kuendelea na elimu ya sekondari itakayokuwa ikitolewa bure hapa nchini.
Wilaya ya Mufindi yenye jumla ya shule za msingi 178 imeshika nafasi ya pili Mkoani Iringa kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwaasilimia 80.39 ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa iliyofaulisha kwaasilimia 80.55 ikiwa na jumla ya shule za msingi 50.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa