Home » » ACT WAZALENDO WASEMA MCHUANO IRINGA NI CHIKU ,MWAKALEBELA NA MASASI ,MCHUNGAJI MSIGWA ASICHAGULIWE KASHINDWA KAZI

ACT WAZALENDO WASEMA MCHUANO IRINGA NI CHIKU ,MWAKALEBELA NA MASASI ,MCHUNGAJI MSIGWA ASICHAGULIWE KASHINDWA KAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Matukiodaimablog
CHAMA Cha ACT wazalendo kimewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu waliojitokeza kuomba kuchaguliwa kupokea  nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)kwa madai kuwa hapaswi tena kupewa kura katika jimbo hilo.

Katibu Wilaya  wa ACT wazalendo Wilaya ya  Iringa Bw Zhenepa Ally leo wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Chiku Abwao ( ACT wazalendo) kwenye kata ya Kitwiru .

Alisema kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa wakati wa Ubunge wake awali alikuwa akipambana na ujangili kwa kupambana na wauwaji wa Tembo na kila mkutano wake alikuwa akionyesha kupiga vita ujangili ila baada ya kushikamana na Waziri Lazaro Nyalandu ( CCM ) kwa kusafiri pamoja katika Ziara za nje aligeuka ghafla na kuacha kabisa kuzungumzia ujangili.

Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu. Waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge jimbo hilo ambalo Mchungaji Msigwa kashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Ubunge ambao wananchi wanapaswa kuwachuja kuwa ni Chiku Abwao ( ACT wazalendo) ,Frederick Mwakalebela(CCM) na Daud Masasi (ADC)na sio kupoteza kura kwa kumpa tena mchungaji Msigwa ambae ametelekeza jimbo hilo kwa miaka yote mitano.

" Katika uchaguzi huu wananchi wa Iringa tunaomba muwapime watu watatu waliojitokeza kumpokea Ubunge Mchungaji Msigwa"

Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo hilo la Iringa Mjini Bi  Abwao alisema jimbo la Iringa Mjini ni moja kati ya majimbo ambayo yalikuwa rahisi zaidi upinzani kuendelea kuongoza tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ila kutokana na kushindwa kwa Mchungaji Msigwa jimbo hilo wananchi wamepoteza imani na upinzani.

Abwao aliwaomba wananchi wa jimbo la Iringa mjini kumchague yeye kuwa mbunge wao kwani sera nzuri za kuwakomboa wananchi hao

" Mbunge  Msigwa aliahidi kuwapa nyavu kwa maana ya mitaji ila kipindi chake chote kaishia kufanya mikutano ya vurugu na kutukana wananchi wake kuwa ni wavivu wanaopenda kucheza bao wakati nae ni miongoni mwa wavivu hao na wacheza bao wazuri"

Hivyo alitaka wananchi wa jimbo la Iringa ili kurejesha heshima ya upinzani jimbo la Iringa Mjini ni wakati wa kuchagua chama cha ACT wazalendo kuanzia Udiwani Ubunge na Urais na sio Chadema kupitia mwamvuli wao wa Ukawa ambao wamesimamisha mgombea ambae yupo katika orodha ya mafisadi.

Akizungumzia kuhusiana na Mgombea Urais wa Ukawa Chiku ,alisema kuwa Mgombea huyo hana sifa ya kuwakomboa watanzania kwani ni genge la walanguzi linalotaka kwenda kutumia Ikulu kwa kurejesha mamilioni ya pesa waliotumia kununua Ikulu.

Hata hivyo alisema watanzania wasidanganyike na safari ya matumaini ya Ukawa kwani safari hiyo haipo tena na hivyo ni vema kuchukua hatua kwa kukataa wagombea hao wa Ukawa.


0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa