Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza mbunge Filikunjombe baada ya kumkabidhi barua ya kupita bila kuingwa ubunge jana
Na Matukiodaima Blog
ALIYEKUWA mbunge
wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe (CCM) amepita
bila kupingwa baada ya
mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)
Barthomew Mkinga kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa
Fomu.
Msimamizi wa Uchaguzi
Wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri alisema
jana
kuwa Mgombea wa Chadema
ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa
Mgombea wa Ubunge hivyo kumkabidhi barua
rasmi Filikunjombe ya
kupita bila kupingwa
Waziri alisema kwamba
Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM,
Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa Wagombea wa DP na
TLP walishindwa kabisa kurejesha fomu
huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha
Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea huyo
wa Chadema aliyereja fomu
ya wadhamini bila
kujaza tarehe ,mwezi wala mwaka ambao uchaguzi mkuu utafanyika .
Kwa upande
wake mgombea ubunge
wa TLP Bw Blanka Haule
alisema kuwa alishindwa kurejesha
fomu hizo kwa wakati kutokana
kukosa picha za kubandika katika fomu hiyo
kutokana na hali ya mazingira
ya Ludewa kukowa
eneo la kupiga picha hizo.
Kwani alisema picha
ambazo alipiga Njombe alizisahau
alikoziweka hivyo kulazimika
kwenda kupiga pich nyingine
za haraka kwa muda
wa dakika tatu ila cha
kushangaza dakika tatu za kutoka
picha hizo zilionekana
kushindwa kutoka kwa wakati na kutoka saa 11
jioni .
“Nilijipanga kugombea
ubunge ili kumpokea
ubunge Deo Filikunjombe na kuendeleza
yale yote aliyoyafanya
jimboni ila watu wa
picha walinikwamisha na kushindwa kupata picha kwa
wakati hivyo kwa sasa ndio
basi tena japo ilikuwa ni Demokrasia lakini kapita bila
kupingwa ndio mbunge wetu:”
Akizungumzia hatua ya
mgombea wao wa Chadema kushindwa
kukamilisha taratibu za
ujazaji wa fomu hizo Bw Daniel Songo alisema kuwa
mgombea wao hakuwa makini hata kidogo kwani alikuwa ni mtu ambae hakutulia
na muda mwingi alikuwa akifikiria juu ya
wanachama wanaohama chama na kuacha kutulia katika kujaza fomu
hizo .
Japo alisema chama hicho kimepoteza
umaarufu kutokana na mwenendo wa
viongozi wa juu wa chama
hicho kuendekeza siasa za ukanda zaidi na kuacha
kutazama uhai wa chama hicho.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanle Kolimba alisema
kuwa amepokea kwa furaha kubwa
hatua ya mgombea wake wa nafasi ya ubunge
kupita bila kupingwa na kuwa kazi kubwa kwa sasa
kuhakikisha mgombea urais wa CCM
Dr John Magufuli anapata kura za
kimbunga pamoja na kupigania
kata zote kuona CCM .
Kwa upande wake
Bw Filikunjombe akizungumzia hatua hiyo ya kupita
bila kupingwa alisema
ameipokea kwa vizuri sana kwa alitegemea wapinzani hao
wajitokeze ili aweze kuwaonyesha kazi kwa
kuhakikisha wanaangukia pua katika uchaguzi huo .
Alisema kazi kubwa ya
maendeleo ambayo ameifanya katika
jimbo hilo kwa miaka mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa
Ludewa wanayo dhidi yake ilikuwa ni
vigumu kwa wapinzania hao kupata
kura Ludewa.
Bw Filikunjombe
aliwaomba wananchi wa Ludewa
kura zote ambazo
walipanga kumpigia yeye
kuzielekeza kwa mgombea Urais Dr Magufuli na kwa madiwani wa CCM
na furaha yake
kuona wapinzani wanaambulia patupu katika
wilaya ya Ludewa .
|
0 comments:
Post a Comment