Home » » MUCOBA YANUFAISHA 33,000

MUCOBA YANUFAISHA 33,000

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BENKI ya Wananchi Mufindi (Mucoba), yenye makao makuu wilayani Mufindi mkoani hapa, imewanufaisha zaidi ya wanachama 33,000 kwa kuwapa mikopo yenye thamani ya sh bilioni 10 kwa lengo la kuanzisha miradi ya maendeleo kwa vikundi.
Akizungumza katika siku ya familia ya Benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Gentle Hill mjini Iringa juzi, Meneja wa Mucoba, Ben Mahenge, alisema kuwa Mucoba imeendelea kuisaidia serikali ya awamu ya nne katika kutekeleza ahadi yake ya ukuzaji wa ajira nchini kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali ikiwa ni kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi kwa ujumla.
“Sisi Mucoba tumeweza kutoa mikopo yenye thamani ya sh bilioni 10 kwa wajasiriamali 33,000 kati ya wanachama 37,000 ili kuanzisha miradi yao ya kiuchumi, hivyo kuisaidia serikali katika kukuza kipato cha mwananchi na nchi kwa ujumla,” alisema Mahenge.
Alisema mbali ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali, benki hiyo imeanza kujipanua zaidi katika mkoa mzima wa Iringa na Mbeya, kwa kufungua matawi mjini Iringa, Ilula na Kilolo na kuanza mkakati wa ujenzi wa tawi jingine katika Wilaya ya Mbarali, Mbeya.
Alisema tangu kuanzishwa kwa benki hiyo, walianza kukopesha kwa watu mbalimbali wenye  kipato cha chini na vyama vya akiba na mikopo (Saccos), vikiwemo vikundi mbalimbali vya kiuchumi sanjari na utoaji wa elimu namna ya kuitumia sekta ya kifedha kifaida zaidi na ukuzaji wa uchumi.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa