Home » » ILO YAWAPA ELIMU YA VVU WACHIMBAJI MUFINDI

ILO YAWAPA ELIMU YA VVU WACHIMBAJI MUFINDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SHIRIKA la Kazi duniani (ILO), kwa kushirikiana na Amref limeanza kutoa elimu ya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu Ihanzutwa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa kuwapa elimu ya upimaji wachimbaji hao na viongozi mbalimbali katika mgodi huo, Ofisa Kazi Mkuu Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana, Amina Likugwala, alisema asilimia kubwa ya nguvu kazi ya taifa ni vijana kati ya miaka 15 hadi 49, ambao ndio wanaoathirika na janga hilo.
Kutokana na hilo, alisema serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, wameweza kuwahamasisha na kuwapata elimu kupima afya zao kwa lengo la kujitambua na kuepuka maambukizi mapya.
Alisema zoezi hilo la kupima VVU mkoani Iringa, limeelekeza nguvu zake kwenye machimbo hayo baada ya kukosa huduma hiyo kipindi kirefu, kwa lengo la kuwafanya wachimbaji hao kutambua afya zao na kuepuka maambukizi mapya.
Likungwala, alibainisha kuna sheria ambayo inaangalia kwamba, mfanyakazi yeyote mahala pa kazi asibaguliwe kwa kuwa na maambukizi ya ukimwi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema yapo maeneo ambayo yanaguswa zaidi katika kupambana maambukizi mapya ya VVU hasa katika machimbo, ambako asilimia kubwa ni vijana wanaotafuta maisha na kupata fedha nyingi endapo wakifanikiwa kupata madini na kusababisha matumizi mabaya ya fedha hasa katika starehe.

Aliwataka vijana kutambua kuwa, pesa ni chanzo cha kufanya jambo lolote ambalo linaweza kukupa majuto, hivyo uhai wa mtu ni haki yake kikatiba lakini uhai huo unatakiwa ulindwe kwa kupewa elimu ya VVU.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa