Home » » TUKIO KATIKA PICHA: HUU NI UBUNIFU MK UBWA NA WA KIPEKEE KUTOKA MKOANI IRINGA! TAZAMA HAPA

TUKIO KATIKA PICHA: HUU NI UBUNIFU MK UBWA NA WA KIPEKEE KUTOKA MKOANI IRINGA! TAZAMA HAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. ubunifu uliotukuka mkoani iringa
Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao


Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake

Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo

Na Francis Godwin, Iringa

Amini usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.

Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.

"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.

"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza kuwa  atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti. 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa