Home » » KISWAGA APELEKA TEKNOLOJIA SHULE YA MSINGI KANING’OMBE IRINGA

KISWAGA APELEKA TEKNOLOJIA SHULE YA MSINGI KANING’OMBE IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kiswaga  akimkabidhi kompyuta  mkuu wa  shule ya Kaning’ombe Bw Mohamed Mchamba (kushoto)
Viongozi  wakifurahia msaada  huo
Mdau  wa maendeleo  katika  jimbo la Kalenga  mkoani Iringa Jackson Kiswaga  ambae ni mkazi  wa  kijiji  cha Nyamihuu amezidi  kusaidia maendeleo ya  wakazi  wa jimbo la Kalenga kwa  kukabidhi msaada  wa  kompyuta na printa katika  shule ya msingi Kaning’ombe .
 
Msaada  huo umetolewa  jana na Kiswaga kama utekelezaji wa maombi ya   wazazi na  uongozi wa  shule  hiyo ambao  mwaka jana  wakati wa mahafali  walimwombe kuwasaidia vifaa hivyo  ili kusaidia  kuchapa na kuprinti mitihani ya  wanafunzi  shuleni hapo.
 
Akizungumza mara  baada ya  kukabidhi msaada  huo Kiswaga  alisema kuwa furaha yake  kuona  wanafunzi  shuleni hapo  wanajifunza komyupta na uongozi wa  shule  hiyo  unapata kitendea kazi kwa ajili ya  kufanyia kazi za wanafunzi.
 
Kwani  alisema  kuwa  kompyuta  hiyo itawasaidia kuchapa mitihani ya  wanafunzi na kuondoa kero kubwa  ambayo  walikuwa  wakiipata  awali kwa  kusafiri  zaidi ya km 30 kwenda mjini Iringa kuchapa  mitihani ya  wanafunzi.
 
Hata  hivyo Kiswaga  alisema kwa  kuwa  eneo  hilo hakuna  umeme na kifaa hicho kinahitaji umeme atawasaidia msaada wa genereta  kwa ajili ya kusaidia umeme katika utumiaji wa  kompyuta  hiyo. 
 
Pia  alisema  akiwa kama mdau wa maendeleo  katika  jimbo  hilo ataakikisha aaendelea  kusaidia  pale ambapo atakuwa na uwezo napo  huku kuhusu maombi ya  wananchi hao  kufikishiwa  huduma ya mtandao wa  simu kwa kufungiwa mnala wa tigo  alisema  kuwa mambi hayo atayafikisha kwa viongozi  wake wa  juu ili kuangalia uwezekano wa  kusaidia japo alisema hawezi  wadanganya kuwa atafikisha mnala huo kesho .
 
Mkuu wa  shule  hiyo Mohamed Mchamba mbali ya  kumshukuru Kiswaga kwa msaada  huo bado  alisema  kuwa  jitihada  kubwa zinazofanywa na mdau huyo ni ukombozi  katika  sekta ya elimu  shuleni hapo.
Kwani  alisema  kuwa  shule  hiyo toka  ilipoanzishwa haijapata  kuwa na kompyuta hivyo msaada  huo ni mkubwa  kwao na kuomba  wadau  wengine  kuzidi kusaidia  shule hiyo 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa