SHIRIKA
la Forum For Africa Women Educationalists (FAWE) linalojihusisha na
utoaji wa huduma za kielimu kwa mtoto wa kike, kupitia mradi wa TUSEME
ambao huwawezesha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujitambua,
kujiamini, kujithamini na kuzitete haki zao, limewakutanisha wanafunzi
wa Wilaya tisa nchini, ili kubaini changamoto zinazowakabiri.
Akizungumza
katika sherehe ya uzinduzi wa kambi ya wanafunzi hao, kambi iliyopo
katika shule ya sekondari JJ Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoni
Iringa, mratibu wa FAWE Tanzania Bi. Neema Kitundu amesema Wilaya
zilizoshiriki katika kambi hiyo ni Temeke, Njombe, Mtwara, Mbeya
Vijijini, Mufindi, Iringa vijijini pamoja na Makete, huku Wilaya ya Magu
na Mbarali zikishindwa kuwapeleka wanafunzi wake katika shughuli hiyo.
Bi.
Kitundu amesema lengo la shirika hilo ni kumuhamasisha mtoto wa kike
aweze kupata elimu bora bila kukwamishwa na vizingiti vyovyote, kwa
kumpa uthubutu wa kuchagua masomo ya Sayansi ili waweze kuingia katika
taaluma mbalimbali kwa usawa baina yake na mtoto wa kiume, huku
likijenga majengo yanayowezesha upatikanaji wa elimu bora, itolewe
katika mazingira rafiki ya elimu kwa jinsia zote.
Mwanzirishi
wa TUSEME nchini Profesa Penina Mlama amesema tangu kuanzishwa kwake
mradi tayari umezifikia nchi 25 barani Afrika huku kukiwa na mafanikio
makubwa katika utoaji wa haki ya elimu kwa mtoto wa kike.
Kaimu
afisa elimu mkoa wa Iringa Mwalimu Ezekiel Kiagho amesema shirika hilo
ni chachu katika sekta ya elimu, kutokana na ukweli kuwa baadhi ya
wazazi na walezi wamekuwa wakiwabagua watoto wa kike katika afua ya
elimu ikiwa pamoja na kumlimbikizia majukumu ya nyumbani na hivyo kukosa
muda wa kujisomea.
Hata
hivyo watoto washiriki Erick Kisima, Irene Nyavanga na Jennifer Steven
Luvanda wamesema katika maeneo ya vijijini bado baadhi ya wazazi na
walezi wanaendeleza ubaguzi kwa watoto wa kike katika suala zima la
elimu, ikiwa pamoja na kumbebesha mzigo wa majukumu ya kazi za nyumbani.
1 comments:
mwanamke ni mtu muhimu sana. Sina maana mwanaume hana umuhimu sana ila wote ni muhimu sana. tukijaribu kuangalia kwenye jamii tunaona mwanamke ndio yupo katika hali hasi karibu kila sehemu, mwanamke ndio mzazi anayelea mtoto, mwanamke anazalisha uchumi kuliko mwanaume. Tembea mashambani msimu huu halafu ujionee idadi ya wakulima na wanawake au wanaume. Kwahiyo kwa hayo machache naona mwanamke anatakiwa kupewa msaada mkubwa kutokana na hali halisi.
Post a Comment