Home » » HOT NUUZ: FRANCIS GODWIN :NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU. AENDA MAFICHONI AKIHOFIA KIFO KABLA HAJATOA USHAHIDI NA KUSEMA UKWELI WA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI!

HOT NUUZ: FRANCIS GODWIN :NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU. AENDA MAFICHONI AKIHOFIA KIFO KABLA HAJATOA USHAHIDI NA KUSEMA UKWELI WA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI!



Mmiliki wa mtandao huu http://www.francisgodwin.blogspot.com Bw.Francis Godwin (kushoto) akitoka kujisalimisha polisi akiwa na mkewe Vumilia Mwangosi (kulia) ambaye ni dadake na marehemu Daudi Mwangosi
Hapa mzee wa matukio daima akiwa na mkewe katika basi
Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa.

1 comments:

JOHN said...

Pole sana Mungu akusaidie.

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa