Mwimbaji Ambwene Mwasongwe |
WAKATI
siku za tamasha kubwa la kihistoria mjini Mafinga mkoani Iringa
zimezidi kusogea ,mkuu wa jimbo la kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) jimbo la Mafinga mchungaji Antony Kipangula ndie
atakayezindua tamasha hilo .
Kwaya ya vijana KKKT usharika wa Iringa mjini siku ilipotembelea bungeni Dodoma |
Akizungumza leo na mwandishi wa habari hizi ,Mratibu wa tamasha hilo Mary
Mungai aliyesa kuwa uzinduzi wa tamasha hilo utakwenda sambamba
na uzinduzi wa ukumbi wa kisasa KWA AJILI ya burudani na shughuli
mbali mbali ukumbi wa MAM ulipo katikati ya mji wa Mafinga na kuwa
washindi wa uimbaji KKKT nchini kwaya ya vijana usharika wa kanisa
kuu Iringa na mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu nchini Ambwene
Mwasongwe wataongoza kupamba tamasha hilo pamoja na kwaya nyingine
na waimbaji binafsi kutoka ndani na nje ya Mafinga .
" kutakuwa na waimbaji wengine mbali mbali pamoja na
burudani nyingine na kuwa lengo la tamasha hilo pamoja na kutoa
burudani kwa wakazi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Iringa na Njombe
bado itakuwa ni siku ya uzinduzi
wa ukumbi wa burudani na sherehe mbali mbali katika mji huo wa Mafinga"
Mungai
alisema kuwa kwa ajili ya kuwashukuru wananchi wa mji wa Mafinga
kwa
ushirikiano mbali mbali ambao wameendelea kuutoa amelazimika kuandaa
tamasha hilo ambalo wananchi watashuhudia kwa kiingilio kidogo
sana kama sehemu ya kuchangia gharama ndogo ndogo za maandalizi ya
tamasha na mchango kwa V.I.P utakuwa ni Tsh 10,000 wakati kawaida
kwa watu wazima ni Tsh 5000 na watoto ni Tsh 3000 pekee na kuwa
ili kuepusha msongamano mlangoni tiketi tayari zinauzwa katika ofisi
ya shule ya Southern Highlands Mafinga , Hazina Bima na
Stationary ya Huruma Msigala na getini pia zitauzwa .
Alisema
pamoja na kuwa wilaya ya Mufindi ni moja kati ya wilaya zenye
uchumi mkubwa hapa nchini na watu wake ni wale wanaopenda
burudani mbali mbali zikiwemo za matamasha ya nyimbo za injili
ila bado kumbi nyingi zilizokuwepo haziwezi kukidhi mahitaji ya
burudani na kuwa kuzinduliwa kwa ukumbi huo kutafungua milango ya
uchumi kwa mji huo kwa wadau kutoka ndani ya wilaya ya Mufindi
na nje ya mkoa kufika kuutumia ukumbi huo kuandaa burudani mbali mbali
na hata kuutumia kwa mikutano mikubwa .
Mwenyekiti
wa kwaya ya vijana usharika wa kanisa kuu Kombo Mdegella
akizungumzia juu ya maandalizi ya ushiriki wao katika tamasha hilo
alisema kwaya yake ambayo imekuwa ikifanya vema katika mashindano
mbali mbali ya uimbaji ipo kwenye maandalizi makubwa ya kuhakikisha
wanatoa burudani ya nyimbo kali kwenye Tamasha hilo .
ukumbi pekee katika mikoa ya
nyanda za juu kusini kujengwa kisasa na utakuwa na majukwaa mawili
moja la kati litakuwa ni jukwaa linalotembea pia kutakuwa na V.I.P
kwa wageni maalum ambao ili waweze kuingia ukumbini watapandishwa
ghorofani kwa ngazi maalum na kushuka kwa ngazi hadi
jukwaani iwapo watataka kutoingilia mlango wa waalikwa wote .
0 comments:
Post a Comment