Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI ya mkoa
wa Iringa imeipongeza kampuni
ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa kushinda tuzo ya (ARSO) kwenye mashindano ya kimaifa ya nchi za Africa ya ubora wa bidhaa za maziwa
kuwa ni tuzo yenye heshima kubwa kwa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla .
Pamoja na pongezi hizo
pia imepongeza jitihada zinazofanywa na kampuni ya Asas Dairies
Ltd kwa kuwawezesha mafunzo mbali mbali wafugaji wa mikoa ya Mbeya , Njombe na Iringa
kubadili ufugaji wa kienyeji na
kufuga kibiashara zaidi
.
Huku ikiwataka
wenye viwanda vya
usindikaji maziwa kujenga utamaduni wa
kuwafikia wafugaji na kuwapa
elimu ili kuwezesha
bidhaa zao za maziwa kuendelea
kuwa zenye ubora
zaidi na ikiwezekana
kuwawezesha kupata vifaa vya kisasa
vya kukamulia maziwa.
Kaimu mkuu wa
mkoa wa Iringa Richard Kasesela
aliyasema hayo leo kwenye ukumbi wa Asas mjini hapa wakati wa
ufungaji wa mafunzo ya wiki moja kwa wafugaji 35 kutoka Iringa ,
Mbeya na Njombe mafunzo yaliyoandaliwa kilimo biashara
yaliyoandaliwa na Shirika la
umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD) kwa ufadhili
wakampuni ya Asas Dairies Ltd
na SAGCOT CTF
Alisema kuwa kampuni
hiyo imeupa mkoa wa Iringa heshima
kubwa na kuwa ukiacha mashindano mbali mbali ya maziwa kwa viwanda vya ndani ya
Tanzania kampuni hiyo
imekwisha shinda mara nne sasa jambo ambalo ni la kujipongeza na
kujivunia kuwa bidhaa zinazozalishwa ni
bora na hivyo si wakati wa watanzania
kukimbilia bidhaa za nje na kuacha zinazozalishwa ndani ya nchi .
Kasesela ambae pia ni
mkuu wa wilaya ya Iringa alisema kuwa mbali ya wadau na wawekezaji waliopo katika wilaya yake na mkoa wa Iringa wamekuwa msaada katika maendeleo ila bado kampuni hiyo ya
Asas Dairies Ltd imekuwa ni
msaada zaidi si tu kwa mambo ya serikali bali hata katika kuwawezesha wakulima na
wafugaji kupatiwa elimu .
Alisema ni vema
wamiliki wa viwanda
kuwa na mbinu ya kuwafikia wafugaji na
kuwapa elimu na mbinu ya
kuongeza kasi ya uzalishaji wa
maziwa bora ili
kuviwezesha viwanda vyao
kuwa na maziwa mengi zaidi na bora na
sio bora maziwa .
Kuwa serikali ya mkoa wa Iringa inatambua
faida ya mafunzo hayo kwa
wafugaji na pia jitihada za
wahisani mbali mbali wakiwemo SAGCOT ,Asas Dairies Ltd na wengine
na kuwa jitihada hizo
zinafanywa na SAGCOT kwa makubaliano ambayo yamefikiwa kati yao na serikali ya awamu ya tano kwa lengo la kuwakomboa wakulima wadogo na wafugaji .
Hivyo aliwataka wafugaji hao ambao wamepewa
elimu hiyo kwenda kuitumia vizuri
ili kufanikisha azma ya serikali ya awamu ya tano kwa kuona
kilimo na ufugaji inakuwa ni
fursa nzuri ya kumkomboa mwananchi .
Kasesela alisema kuwa
kwa mujibu wa tafiti inaonyesha kasi ya
watanzania kunywa maziwa bado
ni ndogo sana kuliko
unywaji wa pombe jambo hali ambayo ni hatari kwa afya
na hivyo ni vema kuendelea kuhamasisha
wananchi kunywa maziwa zaidi
kwa afya zao kuliko pombe ambazo kimsingi
kiafya hazina faida yeyote
mwilini .
Mkurugenzi wa kampuni
ya Asas Dairies Ltd
Ahmed Abri kampuni yake
ilianza mwaka 2000 kwa kuanza
kusindika maziwa kati ya
lita 1000 – 1500 kwa kutengeneza
maziwa mgando na maziwa halisi
baada kuoa bidhaa hiyo
inahitajika zaidi mjini
Iringa walazizimika kuanza
kukusanya maziwa kutoka maeneo mbali mbali ukiacha yale ambayo
yalikuwa yakitoka shambani kwao .
“ Tuliamua
kuanza kuwatembelea wafugaji maeneo mbali mbali
na mwaka 2005 -2006 idadi ya
wafugaji iliongezeka zaidi kufikia
wafugaji 43 hivyo kuanza
kutengeneza bidhaa mpya ya Yoghurt ila bado chagamoto ilikuwa ni maziwa hivyo kulazimika kwenda nje ya
mkoa wa Iringa kama Njombe na Mbeya wilaya ya Rungwe na kuwa
kiwanda chetu kilikuwa na uwezo wa kuzalisha maziwa lita
50,000 kwa siku kutoka
lita 12,000 “
Abri alisema kwa sasa baada ya
kutoa elimu mbali mbali kwa mikoa
ya Iringa ,Njombe na Mbeya hivi
sasa kiwanda hicho
kinawafugaji 1800 ambao
wanapeleka maziwa hapo .
Aidha alisema wakati shirika la afya Duniani linasisitiza
kila binadamu kunywa maziwa lita 200 kwa
mwaka ila kwa watanzania
hata lita mbili kwa mwaka mtu hanywi maziwa na kama atakunywa kwa wingi
basi ni baada ya kuandikiwa na
daktari .
“ Sisi kama kama
kampuni tumekuwa tukihamasisha unywaji wa maziwa na kila mwaka
tumekuwa tukihamasisha
mashuleni na lengo kuona watanzania
wanajenga utamaduni wa kupenda
kunywa maziwa zaidi kwani Tanzania kwa siku inazalisha maziwa lita 300,000 pekee ambazo haziishi sokoni kutokana
na watu kutopenda kunywa maziwa
huku Kenya inazalisha maziwa lita
milioni moja kwa siku na bado
wanalalamika haziwatoshi .
Kuwa maziwa yanayozalishwa nchini ni lita kama 100,000
pekee ndizo zinapelekwa kiwandani na maziwa
yanayobaki yanauzwa mitaani ambayo hayana ubora hivyo rai yao kwa watanzania ni kupenda
kunywa maziwa yaliyosindikwa kutoka
viwandani kuliko kunywa maziwa yasiyo na ubora yanayozungushwa mitaani .
Abri alisema kutokana
na kuzingatia ubora wa maziwa na wafugaji
kuzalisha maziwa bora kampuni
ya Asas Dairies Ltd imeendelea kuongoza nchini kwa
kushinda tuzo za
ubora wa bidhaa zake kwa miaka
minne mfululizo na mwaka huu imeshinda
tuzo nyingine ya mashindano ya kimaifa
ya nchi za Africa tuzo ya ARSO
yaliyofanyika Julay mwaka huu mjini
Arusha yaliyoshinisha makampuni
zaidi ya 60 toka ndani na nje .
|
0 comments:
Post a Comment