Na MatukiodaimaBlog
MKUU
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdulah ametangaza kuwachukulia hatua
kali wananchi watakaopuuza agizo la Rais Dr John Magufuli na
kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila juma la mwisho la
mwezi .
Huku
akipiga marufuku kilimo cha mahindi nje ya ofisi yake kuwa
kuendelea kulima mahindi na mazao yanayozidi futi tatu katika eneo
linalozunguka ofisi yake ni moja ya uchafuzi wa mazingira na kuwa
kuanzia sasa mazao marefu katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za
umma ni marufuku .
Mkuu
huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo juzi baada ya kuongoza
oparesheni ya usafi kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilolo na
wanafunzi wa shule ya sekondari Kilolo kufanya usafi maeneo ya
jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya kilolo jengo ambalo nyoka
walikuwa wakitishia usalama wa watumishi wa ofisi hiyo kutokana na
jengo hilo kuzungukwa na nyasi ndefu na vichaka kwa zaidi ya
miaka 10 .
Akizungumza
baada ya zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza wakuu wa
idara katika halmashauri ya Kilolo pamoja na wananchi ambao
waliitikia wito wa kufanya usafi huku akisema idadi ya
wananchi waliofika kufanya usafi hajafurahishwa nao kwani ni
wananchi wachache ambao walitoka kufanya usafi pamoja na gari ya
matangazo kupita mitaani kabla ya siku ya usafi na kuhamasisha
wananchi kushiriki zoezi hilo .
“Wakati
nikifika
wilayani hapa na kuanza majukumu yangu mapya takribani mwezi
mmoja uliopita kwa kweli sikuridhishwa na hali ya usafi wa mazingira
haya ya ofisi .....nimelazimika kuanza usafi kwanza hapa ofisini
kwangu maana ni hatari hata kwa usalama kama nyoka na wadudu
wengine...hii ni serikali ya hapa kazi Tu hivyo kama mheshimiwa
rais wetu mpendwa Dr John Magufuli alishiriki mwenyewe usafi hivyo
ni lazima kila mmoja kuonyesha kuunga mkono kwa vitendo na sitaacha
kuchukua hatua kwa wote watakaoshindwa kufanya usafi ,”
Bi
Asia alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kuwalenga wananchi wote
kwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake analo ishi kwa
upande wake hakuona sababu ya kuanza kuhamasisha wananchi kufanya
usafi kwenye mazingira ambayo yanawazunguka wakati mazingira
yanayozunguka ofisi yake mkuu wa wilaya kuwa machafu hivyo
alilazimika kuhamasisha wakuu wa idara na walimu pamoja na
wanafunzi kufika kusaidia kuweka mazingira safi katika ofisi
hiyo .
Pia
alisema atawashauri madiwani kutunga sheria ndogo za usafi wa
mazingira itakayotumika kuwawajibisha wananchi watakaoshindwa
kufanya usafi katika maeneo yao na kwa kuanza anawataka wananchi
wote wa wilaya ya Kilolo kuacha tabia ya kupanda mahindi kando ya
nyumba zao kwani ni hatari kwa usalama wao .
Hata
hivyo alisema utamaduni wa wananchi kushiriki uchafu umekuwa ni
mdogo sana katika wilaya hiyo hasa ukitokana na mazoea
yakutoshirikishwa zoezi hilo la usafi ambalo alisema kwa sasa usafi
wa mazingira si kujitakia tena ni lazima kwa wananchi wote
kufanya usafi katika maeneo yao kila jumamosi ya mwisho kwa kila
mwezi na atakayepuuza atawajibika kwa mujibu wa sheria .
Baadhi
ya wananchi walioshiriki usafi katika ofisi hiyo ya mkuu wa
wilaya walieleza kufurahishwa na hatua ya mkuu huyo wa wilaya
kuonyesha mfano wa vitendo kwa kuanza usafi katika mazingira
yanayozunguka ofisi yake ambayo yalikuwa ni machafu zaidi
ukilinganisha na mazingira yanayozunguka ofisi nyingine ama makazi
ya wananchi .
Salome
Kikoti ni mkazi wa Lugalo alisema kuwa mwonekano wa mazingira ya
ofisi ya mkuu wa wilaya yalikuwa ni mabaya zaidi na kuwa hata
watumishi wa ofisi hiyo walikuwepo hatarini kung'atwa na nyoka .
"
Leo wakati tunafanya usafi wa kufyeka nyasi na vichaka katika
eneo hili la ofisi ya mkuu wetu wa wilaya tumeua nyoka mmoja hii ni
dalili ya wazi kuwa kuendelea kuviacha vichaka hivi na uchafu
katika mazingira haya ya ofisi ya mkuu wa wilaya ilikuwa ni
kukaribisha nyoka kuweka makazi yao eneo hili "
Pamoja
na mkuu huyo wa wilaya kufanya usafi katika ofisi yake pia
alishiriki kufanya usafi Zahanati ya Kilolo ,shule ya msingi Kilolo
na katika maeneo ya biashara ya wananchi wa Luganga Kilolo .
|
0 comments:
Post a Comment