Home » » TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba


Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian  Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini Iringa kuhusiana na  ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika  Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16  mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa  maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha  kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.

"Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na  kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa kadi ya kupigia
kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa malalamiko ya
kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye
Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.


Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari


 Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva
akitoa ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika
katika  Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16  mwaka huu.Jaji Lubuvu amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa  maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha  kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa