Home » » WADAI FIDIA YA PARETO

WADAI FIDIA YA PARETO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
mwakilishi  wa  kiwanda  cha  Pareto  Mafinga  Bw Godfrey  Mbeyela  akiwaeleza wananchi  wa Bomalang'ombe  Kilolo faida  ya  kilimo cha  zao la Pareto
Mwamasishaji  wa zao  la  Pareto  nchini Gerald  Chuwa  akiwapa  maelezo  wananchi  wa  Madege kata ya Idete juu ya  faida ya  kilimo cha Pareto
Wananchi  wa Bomalang'ombe  wakimsikiliza  diwani  wa  viti maalum
Wananchi wa kijiji  cha Madege kata ya  Idete  wakiwa  katika mkutano  wa  uhamasishaji wa  kilimo cha zao la Pareto
Wananchi  wa  Madege  wakisikiliza elimu ya  kilimo cha  zao la Pareto
Wananchi  wakitawanyika  katika  mkutano  wa  uhamasishaji  wa  kilimo  cha pareto uliofanyika ofisi ya  kijiji  Madege  Kilolo
Vitalu  vya  miche  ya Pareto  kwa  ajili ya  kupewa bure  wananchi 
 Na MatukiodaimaBlog
WAKULIMA  wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT)  Mafinga kuanza kugawa   bure ya  zao la Pareto .

Akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao La Pareto mwakilishi wa kiwanda cha PCT Bw. Godfrey Mbeyela jana wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bomalang'ombe na Idete , alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata mbegu.

Alisema pamoja na kugawa bure kwa wananchi waliotayari kulima zao hilo la biashara pia kwa wale watakaojiunga vikundi watapewa ajira ya kuotesha miche ya Pareto na kuiuza kwa kampuni ili kuigawa bure kwa wakulima zoezi ambalo litakuwa kwa mwakani

"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"

Juu ya soko la zao hilo ambalo miaka ya nyuma Wilaya ya Kilolo ilikuwa akiongoza kwa uzalishaji alisema kwa sasa soko ni uhakika kwani kampuni  imekuja kwa kasi ya kuwakomboa wakulima na sasa fedha za mazao zitatolewa papo kwa papo shambani baada ya mavuno na hakuna mpango wa kumkopa mkulima .

Pia alisema bei ya zao hilo kwa kilo kwa wananchi wa Kilolo kwa ajili ya kuhamasisha kilo itanunuliwa kati ya Tsh 20000 hadi  Tsh 30000

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.

Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo hekari moja ya Pareto japo mazao mengine waliyozoea yakiwemo mahindi kwa ajili ya Chakula kulima hekari nyingi zaidi.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo alisema kilimo hicho cha Pareto ni fursa kubwa kwa wananchi ambao watachangamkia kuanza kilimo hicho.

Awali wananchi walisema kuwa waliacha kilimo hicho na mashamba ya Pareto kufyeka na kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto ila kwa sasa kwa utaratibu huu mpya wapo tayari kuchangamkia kilimo hicho.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa