Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah wa tatu kushoto akishiriki kupanda miche ya Pareto kwenye shamba la mtaalam wa Pareto Kilolo wakati wa uzinduzi wa kilimo cha Pareto leo |
DC Kilolo katikati akipata maelezo ya miche ya Pareto
Mkuu wa wilaya ya Kilolo na timu ya uhamasishaji wa kilimo cha Pareto wakitoka kutazama vitalu vya miche ya Pareto
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akitazama vitalu vya miche ya Pareto miche ambayo inatolewa bure kwa wakulima
|
Mtaalam wa kiwanda cha Pareto Mafinga Godfrey Mbeyela kulia akishirikiana na Dc Kilolo Asia Abdalah kupanda Pareto |
|
Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ameanza jitihada za kuhamasisha
wananchi wa wilaya hiyo kulima zao la Pareto kama zao la biashara.
Akizungumza
na wananchi wa Udekwa na Lulanzi leo, amesema kuwa Kampeni maalum ya
kuhamasisha kilimo cha zao La Pareto zimeanza leo kwa kupanda Pareto
pia kuona vitalu vya miche ya pareto.
Alisema kimsingi miche hiyo itatolewa bure kwa kila Mwananchi anayehitaji kulima zao hilo.
Alisema pamoja na kupanda mazao mengine ya Chakula na biashara wasiache kupanda japo hekari moja ya zao La Pareto.
Mkuu huyo alisema kuwa zoezi La uhamasishaji upya wa zao La Pareto litafanyika katikati kata mbali mbali za Wilaya ya Kilolo.
Kwani
kati ya Wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao La Pareto kwa mkoa wa
Iringa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao
hilo.
Kuhusu soko aliwataka wakulima kuondoa hofu kwani soko kwa sasa ni uhakika
"Nawaagiza mabwana shamba kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kuwapa Elimu juu ya kilimo cha Pareto"
Alisema
kuwa zao La pareto limekubali sana Wilaya ya Kilolo kutokana na hali ya
hewa ya ubaridi na kuwa zao hilo halihitaji mbolea
Aidha aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi vya kulima zao hilo japo mtu mmoja mmoja anaruhusiwa kulima
"Mimi
mwenyewe nitatafuta eneo La kulima Pareto… ila sisemi muache kulima
mahindi kwenye heka zako 10 tenga heka moja ya Pareto"
Katika hatua nyingine amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mbegu za muda mfupi zaidi.
Mtaalamu
wa Kiwanda cha Pareto Mafinga Godfrey Mbeyela alisema kwa mbegu za
Pareto zimeandaliwa na wanategemea wananchi zaidi ya 40 elfu kulima zao
hilo.
Alisema kwa wilaya ya Kilolo daraja La chini litanunuliwa kwa Tsh 2000 Kwa wakulima wa Pareto Kilolo
Alisema
kuwa soko la Pareto liliyumba kutokana na mwekezaji aliyekuwepo ila
sasa soko lipo La uhakika na kuwa pesa zitalipwa kijijini moja kwa moja.
Alisema kuwa kuwa katika Wilaya nyingine kama Ludewa na Njombe wanagombea kulima zao hilo.
Hivyo aliwaomba viongozi wa dini mbali mbali kutumia Nyumba za ibada kuhamasisha wananchi kulima zao hilo.
Kwa upande wao wananchi wa Kilolo wameeleza kufurahishwa na utaratibu huo wa Kiwanda kugawa miche bure na kuwa wapo tayari kuanza tena kulima zao hilo ambalo awali walikuwa wakilima kwa wingi zaidi
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
0 comments:
Post a Comment