Home » » MUNGAI ASAIDIA YATIMA IRINGA MISAADA YA TSH MILIONI 4.5 KWA AJILI YA SIKUKUU YA KRISMAS

MUNGAI ASAIDIA YATIMA IRINGA MISAADA YA TSH MILIONI 4.5 KWA AJILI YA SIKUKUU YA KRISMAS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  (kushoto ) na mfanyabiashara  Geofrey Mungai wakiwa  wamewapakata watoto yatima  wa  kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi  katika Manispa ya Iringa waliokuwa  wametupwa na  wazazi  wao na kuchukuliwa na  kituo hicho jana  wakati Mungai  alipofika  kukabidhi chakula na nguo za  sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa  watoto hao

Mkuu  wa  wilaya   ya Iringa Bw Kasesela  akisalimiana na Geofrey Mungai kulia 
Bw  Mungai  akiwa na mmoja kati ya  watoto yatima   wanaolelewa  kituo cha DBL
Viongozi mbali mbali  wakiwa katika  picha ya  pamoja na yatima  wa  kituo cha DBL  kutoka  kushoto ni mkurugenzi wa   kituo  hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe , mfadhili Geofrey  Mungai , katibu wa CCM Iringa , mwenyekiti wa CCM Iringa mjini , mkuu wa wilaya  ya  Iringa Bw kasesela,mbunge viti maalum Iringa Ritta kabati ,diwani Dolla Nziku
Mtoto wa  mbunge Mwamoto Leah akitoa ahiadi yake ya  Tsh 50000 kwa  ajili ya  kusaidia yatima
katibu wa CCM Iringa mjini akiahidi  kuchangia  yatima  hao
Mbunge Kabati  akiahidi  kuchangia Tsh 500,000 kwa ajili ya Yatima  hao


Na MatukiodaimaBlog 

WATOTO  yatima  wa  kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi  katika Manispa ya Iringa na  wale  wa kituo  cha Tosamaganga  katika  wilaya ya  Iringa   Iringa    wapewa msaada wenye    nguo  na chakula  msaada wenye thamamani ya Tsh milioni 3 kwa  ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka  mpya .

 

pamoja na msaada  huo wa chakula na mavazi pia  Mungai  aliahidi  kuchangia Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa  vyombo  vya muziki katika  kituo  hicho na kufanya msaada  wake kufikia Tsh milioni 4.5

Huku  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela pamoja na  kumshukuru mfanyabiashara huyo kwa kukumbuka yatima  bado ametoa onyo kali kwa  wanawake  wote  wanaotupa watoto  kuwa   ikibainika watachukuliwa  hatua  kali .

Akizungumza  baada ya  kukabidhi msaada  huo  Geofrey Mungai  alisema   imekuwa ni kawaida  ya  familia  yake  kila mwaka  kusherekea   sikukuu mbali mbali  pamoja na  watoto  yatima kama  sehemu ya  kuikumbusha  jamii  kuwa na  utamaduni  wa  kuwatazama yatima hao  ambao  tegemeo lao  kubwa ni jamii inayowazunguka.

Mungai alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.

Hata hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.

Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama  njia ya  kuwafariji na  kuwalea  watoto hao kuliko  kuwaachia walezi  wao pekee.

Hivyo  alisema  kwa  mwaka  huu  amelazimika  kutoa msaada  wa nguo na  chakula kwa  kila  kituo  msaada  wenye thamani ya  Tsh milioni 1.5 na  kuwa ataendelea  kufanya  hivyo  kwa  ajili ya   watoto  hao ili  siku ya  sikukuu nao  waweze  kufafana  na  watoto   wengine ambao  wanawazazi  wao wote  wawili .


Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe Bw. Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa kituo chake cha  DBL kilichopo  chini ya  usimamizi wa mchungaji Neema Mwaisumbe   kina watoto yatima  43  na kuwa maendeleo ya kituo hicho yametokana na jitihada za wadau mbali mbali ambao wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho.

Alisema kuwa mbali ya familia hiyo ya Mungai kuendelea kutoa msaada wakati wa sikukuu mbali mbali kwa watoto hao bado michango yake imeendelea kuwa chachu kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia  watoto  hao kwa  misaada  mbali mbali .

Hata hivyo alisema kuwa wadau wanaoendelea kusaidia kituo hicho ni wengi zaidi na kuwa kwa umoja wao kituo hicho kinaendelea kuthamini michango yao na kuomba kuzidi kujitolea zaidi kwa ajili ya watoto hao kwa ajili ya  kuona  watoto hao  wanapata  elimu Kituo hicho  ambacho  kina  zaidi ya miaka 15  15 toka kuanzishwa kwake  kimefanikiwa  kuanzisha  shule yake ya  Sekondari  iliyopo  kijiji  cha Mgera ambayo inapokea na  watoto  wengine kwa kuchangia ada ndogo  zaidi kuzindua shule ya sekondari .

kama umeguswa na jitihada za wale wote wanaojitolea kusaidia yatima wa kituo hiki cha DBL mkimbizi Iringa unaombwa kuchangia mchango wako wowote kupitia namba hii ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hiki mchungaji Mpeli kupitia huduma ya TIGO PESA 0719239936 na M-PESA ni 0754362536 na Mungu atakubariki na kukuongezea pale ulipopunguza.

Aidha  alishukuru  ushirikiano  kubwa  ambao  umekuwa  ukionyeshwa na wadau mbali mbali kama mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  ambae amekuwa akijitolea  kusomesha  baadhi ya  watoto  elimu ya msingi kwenye  shule  yake ya  Star  pia  mbunge  wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)  na mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  pamoja na wadau wengine   mbali  mbali .

Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya  ya  Iringa  Kasesela  alisema  kuwa hatapenda  kuona  katika  wilaya  yake watoto  wanaendelea  kutupwa ama  kutelekezwa na  wazazi wao baada ya  kuzaliwa na  kutaka wananchi  kutoa  ushirikiano kwa kuwafichua  wale  wote  wanaotupa  watoto .

Mkuu  huyo  wa wilaya kwa  kushirikiana na  mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa  ajili ya  kuungana na Mungai kusaidianbsp; watoto hao   walichangia  Tsh milioni moja


 

 



0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa