Home » » MTAZAME SAMAKI MKUBWA AINA YA KAMBALE ALIYEVULIWA NDANI YA MTO RUAHA

MTAZAME SAMAKI MKUBWA AINA YA KAMBALE ALIYEVULIWA NDANI YA MTO RUAHA

Mto Ruaha ni moja ya mito ambayo maji yake kwa kiasi kikubwa sio masafi yamechanganyikana na tope, hali hiyo imesababisha kuwa na mazalio  mengi ya samaki aina ya Kambale, Samaki hao ambao wanauwezo wa kuishi kwa muda mrefu hata kama hakuna maji kutokana na kwamba huwa na uwezo wa kujizika ndani ya tope hata kwa miezi zaidi ya sita.
Wavuvi wa eneo hilo wamekuwa wakijishughulisha na uvuvi wa samaki aina mbalimbali lakini zaidi huvua samaki aina ya Kambale, Hivi karibuni wamevua Kambale mkubwa sana na kukili kwamba alikuwa ni moja ya samaki wakubwa ambaye wamemvua.
Wamesema kwamba walisha wahi kuvua samaki aina hiyo mkubwa lakini hakufikia samaki huyo aliyevuliwa hivi karibuni.
"Ni kweli tumekuwa tukivua sana samaki lakini huyu ni samaki mkubwa sana ambaye tumemvu" aliongea Mvuvi.


Huyu ni Samaki Mkubwa ambaye alionekana pembezoni mwa Mto Ruaha Iringa Mara baada ya Kuvuliwa tayari kwa kuingizwa Sokoni.
Samaki huyo akiwa anaonekana kwa ubavuni.

Picha na Iringa yetu

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa