Home » » MRADI WA BILIONI 1.8 KUONDOSHA SHIDA MAJI KATA YA MTWANGO HALMASHAURI YA MUFINDI

MRADI WA BILIONI 1.8 KUONDOSHA SHIDA MAJI KATA YA MTWANGO HALMASHAURI YA MUFINDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Afisa mipango wa Halmashauri isaya Mbenje, akimwonesha Mkandarasi Maeneo mbalimbali  ya kuyafanyia kazi katika chanzo cha Maji cha Sawala.
 Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.8
Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina, kushoto wakimkabidhi Mkataba Mkandarasi Siha Enterprises kulia mara baada ya kusainiwa.
 
Na Afisa Habari Mufindi

Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Kampuni ya Siha Enterprises Limited, kutekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Sawala, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, utakao wanufaisha wananchi wa Vijiji vine vya Kata ya Mtwango baada ya kuikosa huduma ya Maji safi na salama kwa miaka mingi.

Hafla ya kihistoria ya kusaini kandarasi hiyo ya miezi 12, imefanyika katika kijiji cha Sawala mbele ya viongozi wa Vijiji vinne vya Sawala, Mtwango, Lufuna na kibao vinavyotarajiwa kunufaika na huduma hii muhimu kwa uhai wa binadamu.

Akizungunza mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amemtaka Mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa ubora, kukamilisha kwa wakati kadri ya mkataba aliosaini bila kuongeza gharama na ameahidi kuufuatilia mradi huo kwa kila hatua ya ujenzi.

Mh. Jamhuri pia, amewataka wananchi wa kata ya Mtwango kumpa shirikiano Mkandarasi katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi, huku akikemea tabia ya uwizi kwa Vijana watakaopata ajira kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata ya Mtwango.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina, amesema Ofisi yake inaimani kubwa na Mkandarasi huyo na akamtaka aanze kutekeleza ujenzi wa mradi kwa wakati kwani shauku pekee ya watu wa Kata ya Mtwango, ni kupata huduma ya Maji baada ya Mkandarasi wa awali kushindwa kukukidhi shauku yao.

Ujenzi wa mradi wa Maji Sawala, utakelezwa na kampuni wa Siha Enterprises Limited na utasimamiwa na Ofisi ya Maji Mjini Iringa (Iruwasa), Ofisi ya Maji ya Katibu tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa muda usizidi miezi 12. Aidha, baadhi ya shughuli kubwa zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Matenki manne ya ujazo wa lita 450,000, kusambaza mabomba kwenye Vijiji husika pamoja na kujenga vituo 122 vya kukinga Maji.
 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa