Mwimbaji Ambwene Mwasongwe |
Mbunge
wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto katikati aliyevaa tai akiwa na
mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati katika picha ya
pamoja na waimbaji wa kwaya ya vijana KKKT dayosisi ya Iringa
walipotembelea bunge Juni 8 mwaka huu
Na MatukiodaimaBlog
MWIMBAJI
wa nyimbo za injili maarufu nchini Ambwene Mwasongwe na kwaya maarufu
ya vijana wa kanisa kuu la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)
usharika wa Iringa mjini ambayo ni washindi wa pili kiuimbaji Taifa kunogesha tamasha la uimbaji
litakalosindikiza uzinduzi wa ukumbi wa Mam mjini Mafinga .
Mratibu
wa tamasha hilo Mary Mungai alisema kuwa tamasha hilo kubwa la
uimbaji limepangwa kufanyika Desemba 26 mwaka huu ambalo itakuwa ni
siku ya kusherekea sikuuu ya Chrismas ,kutakuwa na waimbaji mbali
mbali kutoka ndani ya mji wa Mafinga ,nje ya Mafinga na kutoka Dar es
Salaam .
Alisema
mbali ya mwimbaji Mwasongwe na kwaya ya vijana kutoka Iringa mjini
ambayo ni kwaya inayofanya vizuri katika nyimbo za injili hapa
nchini pia kutakuwa na waimbaji wengine mbali mbali pamoja na
burudani nyingine na kuwa lengo la tamasha hilo pamoja na kutoa
burudani kwa wakazi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Iringa na Njombe
bado itakuwa ni siku ya MAM Hall itakayokwenda sanjari na uzinduzi
wa ukumbi wa burudani na sherehe mbali mbali katika mji huo .
Hivyo
alisema kwa ajili ya kuwashukuru wananchi wa mji wa Mafinga kwa
ushirikiano mbali mbali ambao wameendelea kuutoa amelazimika kuandaa
tamasha hilo ambalo wananchi watashuhudia kwa kiingilio kidogo
sana kama sehemu ya kuchangia gharama ndogo ndogo za maandalizi ya
tamasha .
Hivyo
alisema mchango kwa V.I.P utakuwa ni Tsh 10,000 wakati kawaida
kwa watu wazima ni Tsh 5000 na watoto ni Tsh 3000 pekee na kuwa
ili kuepusha msongamano mlangoni tiketi zitaanza kuuzwa Desemba 15
katika ofisi ya shule ya Southern Highlands Mafinga , Hazina Bima na
Stationary ya Huruma Msigala
Akielezea
kuhusiana na ukumbi huo alisema ni ukumbi pekee katika mikoa ya
nyanda za juu kusini kujengwa kisasa na utakuwa na majukwaa mawili
moja la kati litakuwa ni jukwaa linalotembea pia kutakuwa na V.I.P
kwa wageni maalum ambao ili waweze kuingia ukumbini watapandishwa
ghorofani kwa ngazi maalum za umeme na kushuka kwa ngazi hadi
jukwaani iwapo watataka kutoingilia mlango wa waalikwa wote .
|
0 comments:
Post a Comment