Home » » MASHINDANO YA MGIMWA CUP YAMEZINDULIWA RASMI NA DC WA MUFINDI JUMHURI WILIAMU

MASHINDANO YA MGIMWA CUP YAMEZINDULIWA RASMI NA DC WA MUFINDI JUMHURI WILIAMU


mkuu wa wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi
 mkuu wa wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji
 mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.

  mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.


na fredy mgunda,iringa. 

MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.

Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri Wiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Wiliamu

Aidha Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.

 “ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Wiliamu
   
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.

“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la mufindi kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema nyimbo

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya mufindi.

“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema kaguo.

Mashindano ya mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa