Home » » MKOA WA IRINGA WATOA SEHEMU YA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI MWAKA 2015

MKOA WA IRINGA WATOA SEHEMU YA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI MWAKA 2015


RC Iringa Amina Masenza 
......................................................................
Na MatukiodaimaBlog 

Ndugu Wananchi wa Mkoa Iringa,
Ndugu Waanishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Nachukua fursa hii kueleza umma kwa muhtasari utekelezaji wa ilani ya ccm ya mwaka 2015 kwa kipindi cha januari hadi juni, 2016 katika Mkoa wa Iringa.Taarifa hii ni sehemu ya utekelezaji ambayo ilianza mwaka 2015.

Ndugu Wananchi, shughuli zilizo tekelezwa kwa kipindi hicho zimefanikishwa kwa kuunganisha nguvu za Serikali kuu,Serikali za Mitaa,Wahisani mbalimbali,Sekta binafsi, Wananchi wenyewe na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.Tunawashukuru wadau wote kwa michango yao.

Ndugu Wananchi, Taarifa hii imetoa maelezo ya utekelezaji na mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi husika kama ifuatavyo;

1. Kuongeza mapato ya ndani IBARA (20)
Mapato ya ndani yaliyokusanywa   ni shilingi 12,767,482,352  ambayo ni sawa na 75.7 ya lengo la shilingi 16,830,702,000   kwa mchanganuo ufuatao;
Kilolo DC 2,180,060,181, Iringa MC 3,526,582,802.93, Mufindi DC 2,837,351,416, Mafinga TC 1,580,742,133, Iringa DC 2,642,745,819

(e) ii Uhamasishaji umefanyika na jumla ya kaya 52,507 zimejiunga na mfuko wa afya ya jamii kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC 9,385, Iringa DC 19,929,Mufindi DC 9,491, Mafinga TC 2,090, Kilolo DC    11,612

2. Kilimo na Ushirika IBARA (22)
(a) Kuongeza upatikanaji wa pembejeo na kusimamia matumizi ya     pembejeo za ruzuku kwa kaya

Halmashauri zote zilipokea pembejeo na kusimamia ugawaji wa pembejeo kwa kutumia mfumo wa vocha ambapo jumla ya vocha 228,000 zimetolewa kwa  kaya 76,000 kwa mchanganuo ufuatao;  Iringa MC vocha 13,680  kwa kaya 4,560,  Iringa DC  vocha 75,240, kwa kaya 25,080, Kilolo DC vocha  57,000 kwa kaya 19,000,Mafinga TC  vocha 22,800 kaya 7,600 na Mufindi DC vocha  59,280 kwa kaya 19,760

(d)ii Kuwezesha vikundi 15 vya Wakulima kuzalisha mbegu za kuazimia ubora (QDS). 
Jumla ya vikundi 9 vya Wakulima wa kuzalisha mbegu za kuazimia ubora (QDS) vimewezeshwa kwa mchanganuo ufuatao; Kilolo DC 4 na Mafinga TC vikundi 4 na Mufindi DC 1

(d)iv Kuimarisha vikundi vya vijana kwa kuvipatia mafunzo.
Jumla ya wakulima 359 wamepatiwa mafunzo ya viuagugu katika Kilimo ambapo kati yao vijana 224 na wanawake 135 kwa mchanganuo ufuatao;
Manispaa -wanawake 97 na vijana 49, Kilolo DC- vijana 127 na wanawake 18 Mafinga TC- Vijana 48 na Wanawake 20.

(g)i Kujenga masoko 2 na maghala 5.
Maghala 2 ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yanaendelea kujengwa ambapo hali ya ujenzi imefikia asilimia 45

3. Mifugo (IBARA25)
(e) Kuanzisha  mashamba darasa 18 ya malisho.
Jumla ya mashamba darasa 15 ya malisho yameanzishwa ili wafugaji wa asili wajifunze jinsi ya kuboresha na kuhifadhi malisho (feed banks) hususan wakati wa kiangazi na ukame kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 1, Iringa DC 7, Mufindi 4 na Kilolo 3

(g) Kutoa elimu kwa wafugaji.
Elimu imetolewa kwa wafugaji 253 kwa mchanganuo ufuatao Iringa DC 93, Kilolo DC 54, Mufindi DC 71 na Mafinga TC 36


4.  UVUVI (IBARA 27)
(K) kuiendeleza Sekta ya Uvuvi
Jumla ya vikundi vitano (5) vya vijana (3) na wanawake (2) vya ufugaji wa samaki vimeanzishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Halmashauri nyingine zinaendelea na uhamasishaji.

(L) Ujenzi mabwawa ya samaki
Jumla ya mabwawa ya samaki 20 yamejengwa kwa  kushirikiana na wadau wa ufugaji samaki ili kuongeza uzalishaji wa samaki kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 1, Mafinga TC 2,Iringa DC  17

5. Utalii (IBARA 29)
(e) Kuongeza idadi ya wananchi wanaotembeela vivutio vya utalii.
Jumla ya Wananchi 1300 wametembelea vivutio vya utalii kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 410, Iringa DC 210, Kilolo DC 320 na Mufindi DC 360
6.  Sekta ya Maliasili(IBARA 29)
(d)ii Kuongeza idadi ya mizinga ya kisasa ya nyuki
Jumla ya mizinga 17,715 ya kisasa ya nyuki imeongeka kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 205, Mufindi DC- 5717, Kilolo DC 7790 na Iringa DC   4,003.


(f) Kuongeza eneo la kupanda miti.
Jumla ya hekta 11,792.65 za eneo la kupanda miti limeongezeka kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC hekta 200, Kilolo DC hekta 11,213, Iringa DC hekta 12 na Mafinga TC hekta 367.6.

7. Sekta ya Ardhi (IBARA 37).
(a)iv Kuongeza upimaji wa viwanja.
Jumla ya viwanja 494 na mashamba 3,778 yamepimwa  kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa   MC viwanja 183, Mufindi DC Mashamba 2124, Kilolo DC Mashamba 475, Mafinga TC viwanja 300 na Iringa DC viwanja 11 na mashamba 1,179.

(a)viii Kutoa elimu kwa Vijiji 360 na Mitaa 222 juu ya Sheria za Ardhi na Sheria ya    Mipangomiji 
Elimu imetolewa kwa Vijiji 19 na Mitaa 9 juu ya Sheria za Ardhi na Sheria ya Mipango miji kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC Mitaa 5 , Mufindi  DC Vijiji 8, Kilolo DC Vijiji 5 Mafinga TC-Mitaa 4 na Iringa DC Vijiji 6.

 (a)ix Kuanzisha na kuyaendeleza mabaraza ya ardhi
Jumla ya Mabaraza ya Ardhi 52 yameundwa ili kufanikisha suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 18, Mufindi 4, Kilolo DC 23, Mafinga TC 5 na Iringa DC 2

8. Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya ardhi nchini (IBARA 37 B)
(b)iv Kuongeza kasi ya utoaji wa Hatimiliki za Kimila
Jumla ya hati miliki za kimila 3,926 zimetolewa kwa Wananchi kwa mchanganuo ufuatao; Mufindi DC 1,882, Kilolo DC 865 na Iringa DC 1,179

(b)v kuongeza kasi ya utoaji wa Hatimiliki
Jumla ya hatimiliki 1460 zimetolewa kwa mchanganuo ufuatao;Iringa MC 1020, Mufindi DC 14, Kilolo DC 67, Mafinga TC  304 na Iringa DC 55

9.  Nyumba (IBARA 37 (C))

(b)ix Kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora
Elimu imetolewa kwa Vijiji 8 na Mitaa 36 juu ya ujenzi wa nyumba bora kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC Mitaa 20, Mufindi DC Vijiji 3, Kilolo DC- Vijiji 5 , Mafinga TC- mitaa 16
10. USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI (IBARA 39)
   (b)ii Kujenga barabara za lami na changarawe
Jumla ya  km 28.06 za kiwango cha lami  na  km 285.5 za kiwango cha changarawe zimetengenezwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC ( lami km 4.09 na changarawe 2.5), Mufindi DC    (lami Km 14.973 na changarawe Km 98) ,Kilolo DC (lami km 1 na  changarawe km.156) Mafinga TC changarawe  km 23 , Iringa DC (Lami km 8 na changarawe km 29)

11. AFYA (IBARA 49)
(a) (i) Jumla ya  Hospitali  mbili (2), zahanati (21) na vituo vya afya (6) vinaendelea kujengwa kwa mchanganuo ufuatao ; Iringa MC Hospitali (1), Kilolo DC Hospitali (1), Vituo vya afya (5) na Zahanati (14). Mafinga TC Zanahati (4 ), Iringa DC kituo cha afya kimoja (1) na Zahanati(3)
12. AFYA (IBARA 50)
(b)i Jumla ya vyandarua 420,545 vimegawiwa kwa Wananchi kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 42,589, Mufindi DC 146,634, Mafinga TC 44,556 na Iringa DC 186,766

(b)v Usambazaji wa dawa umefanyika katika   vituo  159 kwa mchanganuo ufuatao;
       Iringa MC 21, Mufindi DC 62, Iringa DC 76
(P) Jumla ya wazee 17,625 wametambuliwa na  kupewa matibabu bure kwa mchanganuo ufuatao; ; Iringa MC 1386, Mufindi DC 14,558, Kilolo DC 200 na Iringa DC   1,481 
(q)v vituo 105 vimepelekewa Dawa za kupunguza makali ya VVU na vifaa tiba kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 16 , Mufindi DC 22 na Iringa DC  67

13. HUDUMA ZA JAMII (IBARA 52)

(a)i Elimu ya awali
Jumla ya watoto 33,708 wa elimu ya awali wameandikishwa kati ya lengo la kuandikisha watoto 28,712 kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 3,283, Mufindi DC 9,740, Kilolo DC 8,390, Mafinga TC 1,546 , Iringa DC  10,749

(a)i Kuongeza idadi ya madawati
Jumla ya madawati 24,533 yametengenezwa kati ya lengo la kutengeneza madawati 29,347 Madawati hayo yametengenezwa kwa  mchanganuo ufuatao; Shule za Msingi Madawati  21,304 na Shule za Sekondari Madawati 3229,

(a)iii kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la VII wanaendelea na kidato cha kwanza kwa 100%.
Wastani wa 94.5% wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la VII    wamendelea na kidato cha kwanza kama ifuatavyo; Iringa MC 99.02%, Mufindi DC 98%, Kilolo DC  92%, Iringa DC 89.2% .
(d)vi Kuendela kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Sekondari.
Jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule za sekondari kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 8, Kilolo DC 40, Iringa DC 48.
(d)viii Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo shuleni
Mashindano ya yanayohusisha shule za Sekondari (UMISSETA) yamefanyia katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.

 14. Maji (IBARA 54)
(a)Kuboresha huduma ya Maji Vijijini
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama umefika asilimia 71.2 na utekelezaji wa miradi yote ya maji ni kama ifuatavyo;Iringa MC upo phase ya kwanza, Mufindi DC  umefikia 30%. Iringa DC Mradi wa Maji Kikombwe na Weru umefikia 95%, Mradi wa Maji Mfyome umefikia 80%, Mradi wa Maji Malinzinga umefikia 60%
 (b)i Kuboresha huduma ya Maji Mijini.
Uboreshaji na upanuzi wa mitandao ya maji eneo la makao makuu ya Mkoa umefikia asilimia 97.

(b)Viii   Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya utoaji wa majitaka
Halmashauri ya Manispaa inaendelea na kazi ya ujenzi na ugawaji wa wateja kwenye mfumo wa majitaka  kazi hii inafanywa na taasisi ya IRUWASA ambapo imefikia 16.5%.

15. UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI (IBARA 57)
(b)Jumla ya   vikundi  vya ujasiliamali na VICOBA 873 katika  Mitaa 26 na vijiji 41 vimetambuliwa na kusajiliwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 741  katika Mitaa 20, Mufindi DC 83 katika Vijiji 17, Mafinga TC- vikundi  132  katika Mitaa 6, Iringa DC vikundi  49 katika vijiji 24.

(b)ii Kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake  na vijana
Jumla ya vikundi 152  vya wanawake na vijana vimepatiwa mikopo kwa mchanganuo ufuatao;Iringa MC  Wanawake 6 vijana 4, Mufindi DC  wanawake 28 vijana 28,  Mafinga TC wanawake 5, Iringa DC wanawake 41 vijana 40.

(b)iii Kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vikundi  vya wanawake 170,  vikundi 45 vijana
Jumla mafunzo ya ujasiliamali  yametolewa kwa vikundi 243 kama ifuatavyo; Iringa MC-Jumla ya vikundi 17, Mufindi DC wanawake 73 na vijana 17, Mafinga TC wanawake 15 na vijana 6, Iringa DC wanawake 81 na vijana 34

16. KUENDELEZA MAKUNDI MAALUMU (IBARA 165)

Kuwatambua wazee na kuwapa huduma ya matibabu katika vijiji ,mitaa na vitongoji.
Jumla ya wazee 17,625 wametambuliwa na kupewa matibabu bure kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 1386, Mufindi DC 14,558, Kilolo DC 200 na Iringa DC   1,481 
17. WALEMAVU (IBARA 166)
Kuendelea Kuwatambua na kuwalinda walemavu wote wakiwemo wenye elemavu wa ngozi katika vijiji,mitaa na Vitongoji.
Jumla ya walemavu 151 wametambuliwa na kulindwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 22, Mufindi DC 81 na Mafinga TC 48.

18. WANAWAKE (IBARA 167)
Kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote katika vijiji 
Elimu kwa wanawake ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote  imetolewa katika   Mitaa 49 na vijiji 41 kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC Mitaa 38, Mufindi DC vijiji 20, Kilolo DC vijiji 10, MafingaTC Mitaa 6 na Iringa DC  vijiji 11
19. WATOTO (IBARA 169)
Kuendelea kutoa elimu juu ya sheria   ya mtoto ya mwaka ya 2009
Elimu juu ya sheria   ya mtoto ya mwaka 2009 imetolewa kama ifuatavyo; Mafinga TC Mitaa 5, Mufindi DC kata 19.

20. VIJANA (IBARA 171)
Kufanya uraghibishi wa vijana ili waweze kujiari katika nyanja mbalimbali kama kilimo, ufugaji, ufundi sanaa
Uraghibishi wa   Vijana katika nyanja mbalimbali kama kilimo, ufugaji, ufundi sanaa umefanyika    katika Halmashauri zote kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC Kata 10 Mufindi DC- Kata 3, Mafinga TC kata 7, Iringa DC kata 5 kilolo DC kata 1.


CHANGAMOTO KATIKA UTEKELEZAJI

Katika utekelezaji wa ilani kwa kipindi husika Mkoa umeendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zinafanya utekelezaji wake kutofanyika kama ilivyokusudiwa.
·       Uchakavu wa magari ambao unasababisha kuongezeka kwa gharama za kuyahudumia pamoja na uhaba wa vifaa vya kutendea kazi
·       Ufinyu wa Bajeti kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wakuu wa Wilaya na Halmashauri,
·       Ucheleweshaji wa kutolewa kwa fedha na kutotolewa kwa fedha pungufu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo zilizoidhinishwa kutoka Hazina.
Mkoa, umejitahidi  kuchukua hatua mbalimbali katika    kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na;

·       Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri ili kupata fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri husika.
·       Kuendelea kufuatilia hazina fedha ambazo hazijatolewa ili ziweze kutolewa
·       Kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali chini ya mfumo wa PPP (Public Private Partnership) katika kutekeleza shughuli mbalimbali.

 

TISHIO LA KUANDAMANA NA UVUNJIFU WA AMANI

Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa zinatoa wajibu ambao
unavifanya vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa ustaarabu na uadilifu.
Ibara ya 5 ya Maadili hayo inaeleza kama ifuatavyo;
5.–(1)Kila chama cha siasa kitakuwa na wajibu
 wa maadili chini ya kanuni hizi kwa:-
·       kuzieleza kwa wanachama wake ili kuongeza uadilifu wa kisiasa ndani na nje ya chama cha siasa;
·       kulaani, kuepukana kuchukua hatua zitakazofaa ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, uvunjaji wa amani au ukandamizaji wa aina yoyote ile;
·       kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote;
·       kulaani na kupinga
·       matumizi ya lugha ya matusi

Kwa kuzingatia Sheria, kila chama cha siasa kinatakiwa kuwa uhuru kushirikiana na chama cha siasa kingine katika kuwaletea maendeleo wananchi na sio kusababisha vurugu ndani ya eneo Fulani.

Hivi karibuni tumesikia matamko ya viongozi wa kisiasa wakiwataka wananchi kuandamana nchi nzima tarehe 01/9/2016. Kwa mkoa wa Iringa, nawaomba wananchi kuwapuuza viongozi hao. Tuepuke maandamano na badala yake tufanye kazi kwa bidii.  Huu si wakati wa maandamano katika Mkoa wa Iringa.

Nawaomba sana wananchi, tuendelee kushirikiana, tufanye kazi kwa bidii na tuachane na wahitaji wa mitaji ya kisiasa kwa sasa.

Muda wa kutafuta mtaji wa kisiasa ukifika, wataruhusiwa kufanya maandamano. Wakuu wa Wilaya, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, vijiji simamieni suala la amani katika maeneo yenu.

Sitaruhusu watu kuandamana nataka wananchi wote tufanye kazi kwa bidii.

  Mwisho
Mkoa unatoa shukrani za dhati kwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, wahisani mbalimbali, sekta binafsi, Wananchi pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa ushirikiano mzuri waliotupatia kuwezesha kukamilika kwa utekelezaji wa Ilani kipindi hiki.


0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa