Home » » Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi

  
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu

Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiwa na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huu baada ya kuapishwa.

na matias cana,singida 

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi, Kiapo hicho kimejidhihirisha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe. Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati ya mji wa Singida.



Mtaturu amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wanapata maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya, miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa.



Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu kubwa katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo.



"Naenda kusaidiana nao ili kuhakikisha wilaya ina komaa zaidi kimaendeleo na watu wake kuondokana na uduni wa kipato walionao wananchi, wananchi wana uwezo wa kufuga na kulima vizuri jambo ambalo linaashiria kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umasikini".



Amesema Mtaturu Kuhusu wananchi wa Ikungi kukataa kuchangia shughuli za maendeleo kufuatia pingamizi lilichagizwa na mbunge wa jimbo hilo Mtaturu amesema kuwa Utaratibu wa kuchangia maendeleo upo katika dunia nzima nchi mbalimbali za ulaya na kwingineko zimekuwa zikichangia shughuli za maendeleo nchini Tanzania kwa ajili ya wananchi masikini lakini wananchi tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za maendeleo.



Amesema wananchi wa Ikungi hawapaswi kutumika kisiasa huu ni muda wa kufanya kazi ili tusikubali maendeleo yetu kurudishwa nyuma na wanasiasa au watu wachache wenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko maendeleo.



"Huko nyuma kulikuwa na watu wanajitolea kufanya shughuli za mikono kwa kuchangia mawe, tofali au mchanga hivyo mchango huo ulikuwa muhimu zaidi japo asilimia kubwa ya watanzania wanadhani mchango ni pesa pekee"



Ameongeza Mtaturu Katika halfa hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe amemuapisha mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw Jackson Jonas Masaka, Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula.



Aidha mkuu wa Wilaya ya Manyoni hakuapishwa kutokana na kuwa nje ya nchi kikazi tangu alipoteuliwa. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka wakuu wote wa Wilaya walioapishwa kuhakikisha wanasimamia vizuri katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020.



"Nawaomba mkasimamie uadiligu, uaminifu, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri zetu kufutwa"



Amesema Mtigumwe Mkuu huyo Amewapongeza wadau mbalimbali katika Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo. Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016
KAWAIDA. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiwa na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huu baada ya kuapishwa. na matias cana,singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi, Kiapo hicho kimejidhihirisha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe. Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati ya mji wa Singida. Mtaturu amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wanapata maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya, miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu kubwa katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo. "Naenda kusaidiana nao ili kuhakikisha wilaya ina komaa zaidi kimaendeleo na watu wake kuondokana na uduni wa kipato walionao wananchi, wananchi wana uwezo wa kufuga na kulima vizuri jambo ambalo linaashiria kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umasikini". Amesema Mtaturu Kuhusu wananchi wa Ikungi kukataa kuchangia shughuli za maendeleo kufuatia pingamizi lilichagizwa na mbunge wa jimbo hilo Mtaturu amesema kuwa Utaratibu wa kuchangia maendeleo upo katika dunia nzima nchi mbalimbali za ulaya na kwingineko zimekuwa zikichangia shughuli za maendeleo nchini Tanzania kwa ajili ya wananchi masikini lakini wananchi tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za maendeleo. Amesema wananchi wa Ikungi hawapaswi kutumika kisiasa huu ni muda wa kufanya kazi ili tusikubali maendeleo yetu kurudishwa nyuma na wanasiasa au watu wachache wenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko maendeleo. "Huko nyuma kulikuwa na watu wanajitolea kufanya shughuli za mikono kwa kuchangia mawe, tofali au mchanga hivyo mchango huo ulikuwa muhimu zaidi japo asilimia kubwa ya watanzania wanadhani mchango ni pesa pekee" Ameongeza Mtaturu Katika halfa hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe amemuapisha mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw Jackson Jonas Masaka, Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula. Aidha mkuu wa Wilaya ya Manyoni hakuapishwa kutokana na kuwa nje ya nchi kikazi tangu alipoteuliwa. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka wakuu wote wa Wilaya walioapishwa kuhakikisha wanasimamia vizuri katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020. "Nawaomba mkasimamie uadiligu, uaminifu, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri zetu kufutwa" Amesema Mtigumwe Mkuu huyo Amewapongeza wadau mbalimbali katika Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo. Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa