Home » » DC ASIA ABDALAH AANZA KAZI KILOLO KWA KUPIMA UKIMWI

DC ASIA ABDALAH AANZA KAZI KILOLO KWA KUPIMA UKIMWI

Mganga  wa  kituo cha afya  Kilolo  Ephlon Msuva  akimpima  HIV  mkuu  wa   wilaya  ya   Kilolo mkoani  Iringa Bi Asia Abdalaha  ambaye  alitembelea  kituo   hicho  kuhamasisha  zoezi la  upimaji  VVU na  kuona  huduma  zinazotolewa kituoni hapo

 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Bi  Asia  Abdalah  katikati  akiwa na watendaji wa  kituo  cha afya  Kilolo kushoto ni mganga  mkuu wa kituo  hicho Dr  Seleman  Hassan na  kulia  ni  Ephlon Msuva.

Na MatukiodaimaBlog 

MKUU mpya  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa Bi Asia Abdalah ameanza  kazi ya  kumwakilisha Rais Dr John Magufuli  kwa  kupima Virusi  vya  UKIMWI  kama  njia ya  kuhamasisha   wananchi  wa  wilaya ya  Kilolo  kupima  afya  zao .

Akizungumza  baada ya kupima na   kutembelea kukagua huduma  zinazotolewa  kituo cha  afya   cha  Kilolo  leo asubuhi ,mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  kuwa ni  siku  yake ya  pili  ya kuanza  kazi ndani ya  wilaya  hiyo ya  Kilolo ila mbali ya  siku ya  kwanza kufuatilia  utekelezaji wa agizo la Rais Dr Magufuli la madawati  siku yake ya pili  ameamua  kutembelea  kituo  cha  afya  kuona  huduma zinazotolewa  pia kupima HIV kama  njia ya  kuhamasisha  jamii.

Mkuu  huyo  alisema  kuwa mkoa  wa Iringa  kwa  takwimu  zilizopo  unaonyesha  kuwa  ni miongoni  mwa  mikoa  ambayo  ipo  juu katika maambukizi ya  virusi  vya  UKIMWI na  wilaya  yake ya  Kilolo  ni  miongoni  mwa   wilaya  zenye maambukizi  ya  VVU hivyo pamoja na  kutembelea na  kupata maelezo ya  mikakati ya  wilaya  katika  kupambana na maambukizi mapya ya VVU amelazimika  kupima VVU kama  sehemu ya  kuhamasisha  jamii ya  Kilolo na  pia kuonyesha mfano kwa jamii.

“ Nawaomba  wananchi  wa  Kilolo  kujenga  utamaduni  wa  kujua  afya  zao  kwa  kupima VVU pamoja na magonjwa  mengine ambukizi   ili  kuwa na wananchi  wenye  afya  bora “

Alisema  kuwa  serikali  imeweka utaratibu  mzuri  wa  kuwapatia  dawa  wale  wote  watakaobainika   kuwa na maambukizi ya  VVU na  kuwa  lengo ni  kuona  hakuna mtanzania  ambaye anapoteza maisha  kwa  kukosa  dawa hizo  za kupunguza makali ya  virusi  vya  UKIMWI .

Aidha  aliwataka   wauguzi  na  madaktari  katika  wilaya   hiyo  kuendelea  kufanya  uhamasishaji na  elimu kwa jamii  ili  wazidi  kujitokeza  kuchunguza  afya  zao .

Pia alisema  amefurahishwa na  mkakati wa  wilaya ya  Kilolo wa  kujenga  Hospitali  yake ya  wilaya  katika  makao makuu  ya  wilaya hiyo  na  kuwa tayari  wilaya  imetenga  ardhi kwa  ajili ya  ujenzi huo .

Alisema  suala la  kusogeza  huduma  za afya  karibu na  wananchi  ni  moja kati ya  sera   chama cha mapinduzi (CCM) na kwa upande  wake  atahakikisha  ujenzi  huo  unakamilika . 

Kwa  upande  wake Mganga  wa kituo  hicho  cha afya Kilolo Dr Seleman Hassan  alisema  wilaya  hiyo  imekuwa na  mikakati mbali  mbali ya  kupambana na maambukizi ya  VVU na  kuwa wakati wa mbio  za  mwenge  wilayani hapo jumla ya watu  200 walijitokeza  kupima VVU na kati yao  watu 19  waligundulika kuwa na maambukizi ya  VVU  na  tayari  wameingizwa katika  huduma ya  kupewa  dawa  za ARVS

MWISHO

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa