Home » » WAHAMIAJI HARAMU 83 WAKAMATWA TENA IRINGA

WAHAMIAJI HARAMU 83 WAKAMATWA TENA IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
JESHI la polisi mkoani Iringa  limeendelea na msako Mkali dhidi ya wahamiaji haramu baada ya kuwakamata tena Jumla ya wahamiaji haramu Raia wa Ephiopia   83  wakiwa njiani kusafirishwa  kwenda nchi za kusini mwa Tanzania


Kukamatwa kwa wahamiaji hao kumekuja siku chache baada ya wahamiaji zaidi ya 50 kukamatwa katika maeneo hayo wakitokea Ephiopia .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba alisema leo  kuwa wahamiaji  hao waliokuwa wakitokea Pwani Kati yao 83 ni wahamiaji kutoka Ephiopia wakati na wawili kati yao ni Dereva pamoja na Msaidizi wake waliokuwa wakiendesha gari hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kakamba alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika kijiji cha Mahenge  kata ya Mazombe Tarafa ya Mahenge wilayani Kilolo.

 Kamanda Kakamba alisema  kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa ndani ya gari aina ya Scania lenya no. za usajili T478 DFE mali ya mfanyabiashara moja wa jijini mbeya lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda  Wilayani Kiyela Mkoani Mbeya
Alisema baada ya mahojiano na dereva wa gari hilo Hance Mwakyoma na utingo wake Alex Adamu    walilieleza jeshi la Polisi kuwa  waliwapakia watuhumiwa katika kata ya Kongowe Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kwamba walikuwa wakiwapeleka kyela Mkoani Mbeya.


“Watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa tano asubuhi na askari polisi waliokuwa doria katika maeneo hayo wakiendelea na kazi ya oparesheni ya kukabiliana na wahamiaji wasio na vibali,biashara ya binadamu na makosa mengine ya jinai”alisema Kakamba

Kakamba alisema pamoja na kukamata watuhumiwa hao pia wamefanikiwa kubaini mtandao unaotumika kwasafirisha watu hao na kuongeza kuwa wanawasiliana na wenzao ili kuushaghulikia mtandao huo ili kuweza kuutokomeza kabisa .

“Mara nyingi watui hawa wanaofanya biashara hii wamekuwa wakiwa na mtandao mkubwa kwa kuwa watu hawa wamesema wameanzia kongwe lakini kwenge ni Tanzania na hawa sio raiya wa Tanzania hivyo wameyo0ka huko waliko tuka sasa lengo leyi ni kuuwa huo mtandao kabisa maana hawa wakiingia huko mitaani sio watu wazuri kabisa alisema Kakamba.

Kakamba alifafanua kuwa mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao hali zao hazikuwa nzuri kutokana na kutokula kwa muda mrefu na kukosa hewa  kutokana kuwa kwenye gari lisilo na   hewa  jambo lililowalazimu kuwahudumia wahusika hao  ili kurudi katika hali zao za kawaida .

Alisema watuhumiwa watatu hali zao zilikuwa mbaya na kwamba baada ya kufikishwa kituoni walilazimika kufikishwa hosptalini ambako walilazwa na kupatiw amatibabu ikiwemo kuongezewa maji .

Hata hivyo kamanda Kakamba Alisema kuwa watu watafikishwa mahakamani pindi taratibu zatakapokamilika kwa   ushirikiano wa jeshi hilo na kikosi cha uhamiaji mkoani hapa.

Chanzo Matukio Daima 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa