Home » » MBUNGE MWAMOTO AFANYA ZIARA YA GHAFLA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KILOLO ,ASIKITISHWA NA UKOSEFU WA CHUMBA CHA MAITI ASEMA ATAJENGA KWA POSHO ZAKE ZA UBUNGE

MBUNGE MWAMOTO AFANYA ZIARA YA GHAFLA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KILOLO ,ASIKITISHWA NA UKOSEFU WA CHUMBA CHA MAITI ASEMA ATAJENGA KWA POSHO ZAKE ZA UBUNGE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo Bw  Venance  Mwamoto kushoto  akitembelea Hospitali teule ya Ilula leo
Mwamoto  akiongea na Matron wa Hospitali  hiyo
Mbunge  Mwamoto  akitembelea  mawodi ya  wagonjwa  Hospitali teule ya Ilula
Baadhi ya  wagonjwa  wakifurahia ziara za  mbunge Mwamoto
Mwamoto  akionyesha eneo la  kuoshea maiti katika  chumba  cha kuhiafadhia maiti Hospitali teule ya  Ilula
Mwamoto  akitoa maelekezo  kwa viongozi  wa Hospitali  hiyo  kulia ni mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo Bi Anna Msola
Vitendea kazi Hospitalini hapo
Mwenyekiti  wa bodi ya Hospitali  hiyo Bi Anna Msola kulia akimweleza jambo mbunge Mwamoto

Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la  Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto  amefanya ziara ya  kushtukiza katika Hospitali  Ilula ambayo ni Hospitali teule ya wilaya ya Kilolo na kuahidi kujitolea  kujenga chumba  cha  kuhifadhia maiti kitakacho gharimu zaidi  ya Tsh milioni 500 baada ya  Hospitali  hiyo kuwa na chumba  cha  kuhifadhia maiti kidogo kisicho na majokofu maalum ya kuhifadhia maiti.

Mwamoto ambae  aliambatana na mwenyekiti  wa  bodi ya Hospitali  hiyo Bi Anna Msolla alitembelea Hospitalini hapo leo  majira ya saa 6 mchana na  kukutana na mganga mfawidhi  wa Hospitali  hiyo  kabla ya  kutembezwa maeneo  mbali mbali ya Hospitali  hiyo kikiwemo chumba  cha  kuhifadhia maiti na mawodi ya wagonjwa .

Awali mganga mfawidhi  wa Hospitali  hiyo Dr Yumpha Sovelo alimweleza mbunge   huyo  kuwa Hospitali   hiyo inakabiliwa na changamoto  mbali  mbali  ikiwemo ya ufinyu  wa chumba  cha  kuhifadhia maiti  pia  kukosekana  kwa majokofu ya kuhifadhia maiti katika  chumba   hicho ambapo kwa  sasa maiti  zimekuwa  zikilazwa chini na huwalazimu  ndugu kuchukua maiti za  ndugu  zao mapeni  zaidi  ili  kuepuka kuharibika .

Pamoja na Changamoto   hiyo  pia  alisema suala la dawa limekuwa ni kero  kubwa kwani kiasi cha dawa ambacho  wanapatiwa na MSD hakitoshelezi mahitaji ya  wagonjwa katika Hospitali  hiyo ambayo  hutegemewa katika ukanda  huo  wa milima ya Kitonga kutokana na  kutokea kwa ajali za mara kwa mara na majeruhi kukosa dawa .

Alisema  kuwa Hospitali  hiyo  imefunguliwa mwaka 2007 na  changamoto   hiyo  imekuwepo na  kuwa kwa ujio huo wa mbunge ni neema kwa  wananchi  wa Kilolo ambao kutokana na kukosekana kwa chumba cha kisasa  cha  kuhifadhia maiti wananchi  wamekuwa  wakiharakisha mazishi kukwepa  kuharibika .

Hata  hivyo  alisema chumba  kinachotumika  sasa ni mfano  wa  chumba  cha  kuhifadhia maiti  ila kiuhalisia Hospitali   hiyo haina  chumba cha  kuhifadhia maiti chenye ubora .

Akielezea suala la uhaba  wa dawa alisema  kuwa hali si nzuri  sana kwani mfano mwaka jana  waliomba dawa za Tsh milioni 11 ila  waliishia kupata  dawa  za Tsh milioni 6 pekee na kwamba mgao  huo  wanapata kutokana na kukosekana kwa dawa  za kutosha MSD na sio pesa kwa Hospitali   hiyo.

Hivyo  alisema  kutokana na uhaba  huo wa dawa Hospitali  imekuwa  ikiingia gharama kwa  kwenda  kununua dawa katika maduka binafsi ambayo  huuza dawa mara mbili ya bei ya MSD .

Mbunge Mwamoto  mbali ya  kupongeza uongozi  wa Hospitali  hiyo kwa kuwa kazini  wakati  wote na  kuendelea  kuwa na mipango endelevu ya kuboresha mazingira ya Hospitali   hiyo bado  alisema amesikitishwa  zaidi ya ukosefu  wa chumba  cha  kisasa cha  kuhifadhia maiti na kuwa kwa  upande  wake kupitia posho zake  za ubunge na ufadhili  wa  wahisani  wa ndani ya  mkoa wa Iringa atahakikisha anajenga chumba   hicho  cha  kuhifadhia maiti ili  kusaidia  wapiga  kura  wake na kero kubwa ya kufanya mazishi ya ghafla ama  kutumia gharama  kubwa  kwenda kuhifadhi maiti Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa mjini Iringa .

Aidha  alisema Hospitali  hiyo awali  ilikuwa ni Hospitali ya kawaida   chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya  Iringa kabla ya serikali kuichukua na kuifanya kuwa  Hospitali teule ya wilaya na kuwa miaka 10  iliyopita  akiwa mbunge alifika  hapo akiwa na  waziri wa afya wakati huo Dr Hussen Mwinyi na  kumwomba  Hospitali  hiyo kuwa  hospitali teule jambo ambalo lilifanikiwa .

Ila alisema moja ya   sifa ya  kuwa Hospitali teule ya  wilaya ni pamoja na  kuwa na chumba  cha  kuhifadhia  maiti japo ilikuwa ikiendeshwa bila kuwa na chumba  hicho na wakati  akiwa katika mchakato ndipo  alipopokelewa kijiti na mbunge mwenzake na hivyo  kuwa nje ya ubunge na  kushindwa kujenga chumba   hicho ila kwa  kuwa amerudi atahakikisha anajenga chumba   hicho .

Akishukuru  kwa ahadi  hiyo ya  mbunge  kujenga chumba  cha  kuhifadhia maiti ,mwenyekiti wa bodi ya Hospitali   hiyo Bi Msolla alisema kuwa ujenzi huo  utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa Hospitali  hiyo na  wananchi  wa Kilolo ambao wamekuwa  wakifanya mazishi ya  kushtukiza  kutokana na kukosekana kwa  chumba  cha  kuhifadhia maiti .
Chanzo Matukio Daima




0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa