Home » » MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA UJENZI WA DARASA LA CHEKECHEA , ASEMA RAIS DR MAGUFULI KAFUTA ADA NA MICHANGO SIO MICHANGO YA UJENZI WA SHULE

MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA UJENZI WA DARASA LA CHEKECHEA , ASEMA RAIS DR MAGUFULI KAFUTA ADA NA MICHANGO SIO MICHANGO YA UJENZI WA SHULE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo  Bw  Venance Mwamoto akikabidhi  fedha  akisi cha Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 alizoahidi kuchangia ukarabati    wa darasa la chekechea kijiji  cha Isele kata ya  Ilula 

...........................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa  jimbo la Kilolo  mkoani Iringa Bw  Venance  Mwamoto achangia  kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuwaunga mkono  wananchi  wake kijiji  cha Isele kata ya Ilula  wilaya ya  Kilolo ambao  wamejitolea  kufanya ukarabati wa darasa la  chekechea kwa lengo la  kusogeza elimu kwa watoto  kijijini hapo.

Huku  akiwataka  wananchi  wote  kuendelea  kuchangia ujenzi  wa vyumba  vya madarasa ,shule na nyumba  za  walimu na kuwa serikali ya Rais Dr John Magufuli  imefuta ada na michango na  sio uchangiaji wa ujenzi .

Akikabidhi  kiasi cha Tsh  500,000 kati ya Tsh milioni 1  ambayo amepanga  kuwachangia wananchi hao leo  mbunge  huyo  alisema  kuwa baada ya  kufika kuhamasisha wananchi kuchangia  shughuli za  kimaendeleo zikiwemo  za  elimu  alikutana na changamoto ya ukosefu  wa darasa la awali katika  kijiji  hicho na  hivyo kuwahamasisha  wananchi  kuanza kutatua  tatizo  hilo.

Bw  Mwamoto  alisema  kuwa baada ya   kufika katika  kijiji   hicho   uongozi  wa kijiji  ulimtembeza  eneo hilo ambalo  wananchi walikusudia  kufanya  ukarabati  wa darasa kwa ajili ya wanafunzi  wa  chekechea  na kuwa mahitaji yote pamoja na nguvu  za wananchi ilikuwa  ni Tsh milioni 2 na hivyo kulazimika  kuchukua  mzigo wa kuchangia pesa kiasi hicho  cha Tsh milioni 1

" Kimsingi hali ya  darasa  lile haikunifurahisha  hivyo  niliwataka  kufanya marekebisho  ili  watoto hao  kuweza  kusoma katika mazingira  bora  zaidi na hii  pesa nimetoa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo na pindi  wakimaliza nitamalizia  pesa  iliyosalia "

Hata    hivyo mbunge  Mwamoto  aliwataka  wananchi  kuendelea  kuchangia shughuli za kimaendeleo hasa  elimu na  kuwa  serikali ya Rais Dr John Magufuli  imefuta michango na ada kwa elimu ya msingi na sekondari  na  sio kwamba imefuta michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ama shule .

Hivyo  aliwataka  wananchi  kuendelea jitihada zao  za  kushiriki  kuchangia maendeleo ya  elimu kwa maana ya ujenzi  wakati  serikali  imechukua  jukumu la kuwalipia  watoto  hao ada na chakula kwa shule za  sekondari za bweni ambazo zipo chini ya  serikali.

Alisema  kuwa  yeye kama mbunge  wao kamwe hata  waacha yatima  katika shughuli  yoyote ya kimaendeleo atahakikisha anashirikiana na  wananchi hao  kikamilifu katika  kuitekeleza .

Afisa  mtendaji wa kata ya Ilulu  Bw  Chusi Ashrafu akimpongeza mbunge Mwamoto kwa kuunga mkono  nguvu za  wananchi hao alisema  kuwa hadi sasa mwitikio  wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo ya umaliziaji wa madarasa  hayo  ni nzuri .

Alisema hadi sasa wananchi  wa  vitongiji  vyote  vitatu wameonyesha  ushirikiano mzuri zaidi kwa  kila kitongoji  kuchangia kiasi cha Tsh 200,000 na  wana jumla ya Tsh 600,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo wananchi  walipaswa  kuchangia wakati mbunge akiahidi kuchangia Tsh milioni 1 na kwa  sasa mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo pia ameahidi kumuunga mkono Mbunge Mwamoto kwa kuchangia Tsh 200,000 hivyo wanamatumaini  kasi ya  ujenzi  huo hadi  sasa imefikia pazuri  zaidi.


0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa