Home » » SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAZIDI KUFANYA VIZURI KIWILAYA HADI TAIFA YASHIKA NAFASI YA KWANZA

SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAZIDI KUFANYA VIZURI KIWILAYA HADI TAIFA YASHIKA NAFASI YA KWANZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Wanafunzi  wa shule ya  Southern Highlands Mafinga wakiwa katika mahafali  yao  ya  14  Mwaka jana
Na MatukiodaimaBlog
MKURUNGENZI  mtendaji  wa  shule ya  Southern  Highlands Mafinga  mkoani Iringa Bi Mary  Mungai amewapongeza walimu  na  wafanyakazi  wa  shule hiyo kwa kuiwezesha  shule   hiyo  kuendeleza rekodi  yake ya  kufanya vizuri katika matokeo  ya  mtihani  wa Darasa la Saba  kiwilaya  ,kimkoa na hata  Taifa  kwa  miaka zaidi ya 13  sasa.

Bi  Mungai  alitoa pongezi hizo  kwa  walimu   wakati akielezea mafanikio  ya  shule   hiyo leo   kuwa kwa  mwaka  huu shule   hiyo  imeweza  kuongoza  tena  kiwilaya  kwa kushika nafasi ya  kwanza  kati ya shule 171 zilizopo wilayani Mufindi na shule  ya  7 kati ya shule 467 katika  mkoa  wa  Iringa na  kitaifa kuwa  shule ya 888 kati ya  shule 16,096

Hata  hivyo  alisema  kuwa  kwa mwaka  jana  shule  hiyo  ya  Southern Highlands Mafinga  ilikuwa nafasi ya  kwanza  kiwillaya kati ya  shule 167 na  kimkoa  ilikuwa ya 8  kati ya shule 458 na  kitaifa  ilikuwa  nafasi ya 353 kati ya  shule 15,867  kuwa matokeo  ya mwaka  huu yameonyesha  ni kwa  kiasi gani  jinsi walimu  wa  shule   hiyo  walivyoendelea kujituma  zaidi katika  ufundishaji .

Alisema  kuwa matokeo hayo ya darasa la  saba  katika  shule   hiyo yanaonyesha ni kwa  kiasi gani walimu  wanavyoendelea kuifanya  shuler hiyo kutoa elimu   ubora   na  sio  bora  elimu hivyo kuwafanya   wazazi  waliowengi kuendelea kuchagua  shule  hiyo kwa  ajili ya  kuwapatia   elimu  bora.

Mkurugenzi  huyo alisema siri  kubwa  ya  walimu  kufanya kazi vizuri  inatokana na  ubunifu  wa safu ya  uongozi  wa  juu  wa  shule hiyo kwa  kuwapa motisha  walimu kila  mwaka pindi wanapofanya vizuri katika  mitihani na  kwa  wanafunzi pia  wamekuwa  wakipongezwa toka wanapoanza darasa la  awali hadi wanapomaliza pindi  wanapofanya vizuri  katika  mitihani  yao.

Alisema  kuwa  shule  ilianzishwa  mwaka 1994 kama chekechea  kwa  jina  la  Lusungu Day Care Center ,Mwaka  1997 ilikuwa na  kuanza shule  ya  msingi  -primary  school ndiyo sasa  inaitwa  southern Highlands yenye  usajili  wake  namba IR03/7/001 ya  mwaka 1997 ambapo  imekuwa  ni  shule  ya pili kufunguliwa  baada ya  Brook Bond


“ Uongozi  wa  shule  umekuwa ukihakikisha  unakuwa na  mpango endelevu  wa  kuboresha mazingira  ya  shule pamoja na  kuboresha  elimu  zaidi ili  shule  hiyo  kuendelea  kubaki  ya mfano  katika taalum mkoa  wa  Iringa na nje ya  mkoa wa Iringa"

Aidha alisema  kuwa mbalia  ya  wanafunzi  wa  shule hiyo kuwa na utaratibu wa kufundishwa masomo mbali mbali  darasani ila  bado  shule  imekuwa na utaratibu  wa  kuwapeleka   wanafunzi katika mafunzo maeneo mbali mbali yakiwemo  ya  vivutio vya utalii katika Tanzania  bara na  visiwani  lengo  likiwa ni  kukuza uelewa  zaidi wa  watoto  hao.

Bi Mungai alisema  kuwa  mbali ya kutembelea  maeneo mbali mbali ya  nje ya mkoa  pia  shule  imekuwa na utaratibu  wa  kuwapeleka  kujifunza  pia katika mashirika  yaliyomo ndani ya mkoa wa Iringa na Njombe .

alisema  ushirikiano mzuri  ambao  wazazi  wamekuwa  wakionyesha  katika  shule  hiyo  hivi  sasa tayari  shule   hiyo imeanzisha   shule ya  sekondari   ambayo  inawawezesha  wanafunzi hao  kuendelea  na  elimu  ya  sekondari na kama  njia ya  kuondoa  usumbufu  wa  wanafunzi  kukosa nafasi  za  sekondari pindi  wanapofaulu .

Kwa  upande  wake kaimu  afisa  elimu  wa  Nasibu A. Mengele  alisema  kuwa  kati ya  shule ambazo  zimekuwa  zikiupatia  sifa  mkoa  wa Iringa kwa kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la  saba ni pamoja na shule  hiyo ya Southern Highlands Mafinga   hivyo wao kama  viongozi wa elimu  wataendelea kuitolea  mfano shule  hiyo kila sehemu na ikiwezekano kuitangaza  zaidi  ili  wazazi  kusomesha  watoto  wao katika  shule hiyo.

Mwalimu  mkuu  wa shule  hiyo Bw Joson Nyang'wara alisema  kuwa jumla  ya  wanafunzi 51  ndio  waliofanya mtihani  wa  darasa  la  saba  na  wanafunzi  wote  wamefaulu katika mtihani  huo hivyo  alisema   kuwa suala la  wanafunzi hao  kukosa nafasi halipo kwani tayari shule   hiyo ya Southern Highlands Mafinga imekwisha kamilisha shule  yake ya  sekondari ambayo  imeanza   kazi toka mwaka jana.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa