Home » » MWAKALEBELA AKANUSHA KUFUTWA KWA KESI YAKE DHIDI YA MCHUNGAJI PETTER MSIGWA NA MKURUGEZI WA MANISPAA YA IRINGA.

MWAKALEBELA AKANUSHA KUFUTWA KWA KESI YAKE DHIDI YA MCHUNGAJI PETTER MSIGWA NA MKURUGEZI WA MANISPAA YA IRINGA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 FREDRICK MWAKALEBELA AKIWA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM  WILAYA YA IRINGA MJINI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
 BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI IRINGA WALIPOKUWA WANAWASIKILIZA FREDRICK MWAKALEBELA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM WILAYA YA IRINGA MJINI.


Chama cha mapinduzi wilaya ya iringa mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya mkurungenzi wa manispaa hii pamoja na mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji PETTER MSINGWA.

akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.

“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015 haijafutwa”alisema Elisha mwampashe.

Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani

“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la msingi  ambalo lilikuwa na kupinga matokeo na kuna  shauri dogo  namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha mwampashe.

Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi  na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwa na subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii wananchi wanaopotosha taarifa hizi.

 kwa upande wake fredrick mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.

“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na mkurugezi wa manispaa ya iringa pamoja na mchungaji petter msingwa” alisema Fredrick mwakalebela 

Mwakalebela amemalizia  kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio kilichompa nafasi ya kugombea ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo. 

ilitolewa taarifa Kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa Mjini Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema kesi ya aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la kuomba kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo.

Hii ni kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo.


Hivyo uvumi uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado haijapangwa wala kuanza kusikilizwa.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa