Home » » WANAWAKE WAASWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI

WANAWAKE WAASWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



 
Wanawake wameaswa kukipenda chama cha mapinduzi kwakuwa ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo yanayotakiwa kwakuwa kinajua changamoto zinazo wakabili wananchi katika kipindi hiki. 

Akizungunguza na  wanawake wa wa Kata ya Makolongoni Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Rose Tweve  aliwataka wananchi kutobabaishwa na wapinzani kwani hawana nia njema na watanzania  na kusema kuwa chama hicho kina misingi ya kutetea amani ya Nchi.
"sisi sote ni wanawake niwaombeni sana tukipigie kura chama cha mapinduzi kiweze kupata ushindi wa kishindo leo katika chama kuna mgombea mwenza mwanamke tazama hamsini kwa hamsini wahamasisheni vijana wenu pia waelezeni mazuri yalimo ndani ya ccm bila kuwaambia wataendelea kurub uniwa na kutumiwa kwa faida za wachache" alisema rose
 
Alisema huu ndiyo wakati wa wanawake kujitokeza kwa wingi kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na chama hicho kwakuwa kukipa nchi chama cha Upinzani ni kujisaliti wenyewe hiyo aliwaomba wanawake kuhakikisha wanakisaidia chama cha mapinduzi kiweze kushinda.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa