Home » » MONICA MBEGA ; DR MAGUFULI NA MWAKALEBELA NAWAUNGA MKONO KWA ASILIMIA 100

MONICA MBEGA ; DR MAGUFULI NA MWAKALEBELA NAWAUNGA MKONO KWA ASILIMIA 100

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Aliyekuwa  mgombea wa nafasi ya Urais Monica Mbega jukwaani  akimwombea  kura  mgombea  urais wa  CCM na mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela (aliyekaa katikati kulia) leo  baada ya  mwakalebela  kuchukua  fomu ya ubunge
Monica Mbega  akimwombea  kura  mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini leo
Monica  Mbega  akimpongeza  Mwakalebela
Monica  Mbega  akijiandaa kumsalimia Kiponza
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw  Abeid Kiponza  (kulia) akimtambulisha mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela  leo
Mwakalebela  akizungumza na  wana CCM leo
Mgombea udiwani wa kata ya Mtwivila Bw Jose Mgongolwa (kulia) akitambulishwa na Mwakalebela
Mgombea  udiwani Bw Chatanda  kulia  akitambulishwa na Mwakalebela
Mwakalebela akimtambulisha Ibrahim Ngwada (kulia) mgombea udiwani kata ya Mshindo
Mgombea  udiwani  wa  kata ya Mvinjeni akitambulishwa
Mgombea  udiwani wa kata ya Mkimbizi Bi Farida Mpogole  akitambulishwa na Mwakalebela
Mwakalebela  akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Bw Nicholina Lulandala
Mwakalebela  akimtambulisha mgombea udiwani wa Kwakilosa Bw Himid Mbata (kulia)
Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Iringa mjini Bw Abeid  Kiponza  akimtambulisha  mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia  CCM Bw  Frederick Mwakalebela (kushoto)
........................................................................................
Na MatukiodaimaBLog
 
ALIYEKUWA mmoja  kati ya  wagombea  wa nafasi ya  urais  kupitia  chama  cha mapinduzi (CCM) na mbunge  wa zamani wa jimbo la  Iringa mjini Bi  Monica  Mbega amesema  kuwa mbali  ya kuwa  yeye  alikuwa ni mmoja kati ya  walioomba kuteuliwa  kuwania nafasi ya  urais na  jina lake  kukatwa bado hana  kinyongo na mteuliwa  wa CCM Dr  John Magufuli kwani anamkubali kwa  asilimia 100 kuwa ni chaguo la watanzania kama  ilivyo  kwa mgombea  ubunge  wa CCM jimbo la Iringa mjini Bw  Frederick Mwakalebela .

Mbega  ambae  alikuwa ni mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini kwa  vipindi  viwili kati ya   mwaka 2000  -2010 alitoa kauli  hiyo  leo   wakati akizungumza na  wanachama  wa CCM katika  viwanja  vya CCM wilaya ya  Iringa mjini wakati  wa mgombea  mteule wa  ubunge  jimbo hilo la Iringa mjini Bw Mwakalebela  kutoka  kuchukua fomu  kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya  kuwania  ubunge kupitia  CCM.

Alisema  kuwa katika  mchakato wa ndani ya  chama wa  kuwania kuteuliwa  kugombea  Urais yeye  alikuwa ni kati ya  wanachama zaidi ya 40  waliojitokeza kuchukua fomu akiwemo Dr Magufuli na  kuwa baada ya  vikao  vya  juu vya  chama  kukamilisha taratibu za  kumpata  mgombea mmoja hakuwa na kinyongo  cha  kuhama  chama  wala kukaa nyuma katika mambo ya chama na ndio maana ameamua  kurejea nyumbani kwake  ili  kuungana na  wana CCM kurejesha  jimbo  hilo kwa  CCM na  kuwapigia kampeni wagombea wote wa CCM akiwemo mgombea  wa nafasi ya urais Dr  Magufuli na madiwani pia.


"Kweli  nawapongeza  sana wananchi  wa  Iringa mlinipa udhamini wa kutosha  wakati wa mchakato wa kuomba  kuteuliwa  kuwa mgombea  Urais wa CCM nilipata  watu 45 kati ya 35  waliokuwa  wakihitajika kweli ni  watu  wengi  sana na baada ya  mchakato  jina langu halikupitishwa na jina la mwenzetu Dr Magufuli ndie  aliyeteuliwa na kazi  yetu ni  kumuunga mkono kwani  kati ya  watu wote  41  ni nafasi mmoja pekee ndio ilitakiwa ....hivyo hakuna haja ya  kuwa na kinyongo kwa  kuhama  chama chetu "


Mbega  aliwataka  wana CCM jimbo la Iringa mjini kuweza kuunganisha  nguvu  zao kwa mgombea  ubunge Bw Mwakalebela ili  kuweza kulikomboa  jimbo  hilo na  kuhakikisha mgombea Urais na madiwani   wa CCM wanapata  kura  za  kishindo  zaidi katika  jimbo la Iringa mjini .

Alisema  kwa  wanachama wa CCM ambao  waligombea nafasi mbali mbali na kura  kutotosha katika nafasi  walizoomba wanapaswa  kuvunja makundi  yao na  kuunganisha nguvu  zao kwa wale  walioshinda  ili  kufanya kazi ya  kujenga  chama badala ya  mtu .

Hata  hivyo  alisema kwa upande  wake atapambana kwa nguvu  zote  kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa katika  jimbo  hilo la Iringa mjini na kudai  kuwa  kazi kubwa  iliyopo mbele kwa  wana CCM ni kujenga utamaduni  wa  kusamehe na kusonga  mbele.

Katibu  wa  CCM wilaya ya  Iringa mjini Elisha Mwampashi akimkaribisha  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza  kumtambulisha rasmi mgombea  ubunge wa jimbo  hilo ,alisema  kuwa ni  lazima  watanzania na  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  kuwapuuza  wale  wote  wanaohama  CCM mara  baada ya  kushindwa katika  kura  za maoni na kuwa watu hao  hawana mapenzi  mema na Taifa  bali  wapo kwa ajili ya maslahi yao  zaidi .

Mwampashi  alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona UKAWA  ambao  walikuwa mbele  kupinga vitendo  vya ufisadi na kumtuhumu  wazi wazi waziri  mkuu mstaafu Edward  Lowasa  kuwa  si  mtu msafi  leo  wamempokea na kuwa mgombea  wao wa nafasi ya urais jambo ambalo  watanzania  wanapaswa  kujiuliza  juu ya mwenendo wa UKAWA katika Taifa  hili.

Mwenyekiti  wa CCM Iringa mjini Bw  Kiponza  alisema kuwa kazi kubwa ya CCM jimbo la Iringa mjini ni  kulikomboa jimbo  hilo  kutoka kwa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Peter  Msigwa (chadema) ambae hakuna  maendeleo  yoyote  aliyoyaleta katika  jimbo  hilo kwa kipindi  chote cha miaka  mitano  zaidi ya wana Iringa  kusababishiwa kupigwa mabomu na lugha  zisizofaa majukwaani .

Hivyo  alisema wana Iringa wanayosababu ya  kusema basi kuendelea  kukosa maendeleo na  kufanya maamuzi  sahihi ya  kukirejesha  chama cha mapinduzi madarakani kwa kumchagua mchapa kazi Bw  Mwakalebela ambae  kwa  muda  wake  mfupi  wa ukuu  wa wilaya ya wanging'ombe kazi kubwa amepata  kuionyesha na hivyo ni zamu ya  wana Iringa  kushuhudia maendeleo  hayo kwa  kumchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo .

" Toka  ameondoka  Mbega mwaka 2010  kwa  kuanzisha  miradi ya barabara na maji ya JR hakuna mradi  ulioendelea  chini ya  ubunge wa Msigwa  zaidi ya maandamano na mabomu kila  wakati na kupinga  wananchi  kushiriki katika shughuli za kimaendeleo"

Kwa  upande  wake mgombea  huyo wa ubunge  jimbo la Iringa mjini Bw  Mwakalebela  alisema kuwa  chini ya ilani ya  CCM serikali imefanikiwa  kuleta maendeleo  kila kona ya nchi hii na hadi sasa  wapo  wanaopinga  kuwa akili ndogo haiwezi  kutawala akili kubwa ila ukweli upo  wazi  kwa  wana Iringa  kuona kasi  kubwa ya miradi ya maendeleo  iliyoletwa na CCM inayoongozwa na wenye akili ndogo kama  mbunge wa  jimbo  hilo anavyojinasibu majukwaani na kuwa haja ya  wananchi kumhoji mwenye akili kubwa ni ahadi gani aliyoahidi ambayo amepata  kuwatimizia  wananchi  wake .

Mwakalebela  alisema  kuwa ni  wakati mzuri kwa wana Iringa  kupima akili ndogo na kubwa katika maendeleo na  sio katika majukwa  ya  siasa na mwisho wa  siku shughuli  za maendeleo  zinasimama na wananchi kushuhudia maandamano kila uchwao .

Alisema  kuwa  iwapo  wananchi  wa Iringa  watamchagua kuwa mbunge wa  jimbo  hilo Octoba 25 mwaka  huu  wawe na matumaini mapya ya  kimaendeleo   ikiwa ni pamoja na  kuanzisha mfumo mzuri wa  kuwakomboa  wanawake na vijana  kiuchumi kwa  kuwapa  mikopo nafuu.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa