Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Bw Frederick Mwakalebela kushoto akiwa ameongozana na katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Elisha Mwampashi
Mwakalebela kushoto akimnadi amgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa Bw Hamid Mbata |
Na MatukiodaimaBlog
CHAMA
cha wazee wilaya ya Iringa mjini kimesema kuwa kutona na mbunge
aliyemaliza muda wake jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
(Chadema) jimbo hilo kwa sasa wanatamani kuona linarudi kwa
mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Bw Frederick Mwakalebela .
Katibu
wa chama hicho cha wazee wilaya ya Iringa mjini Edson Sanga
alisema hayo katika viwanja wa CCM wilaya ya Iringa mjini
kuwa jimbo hilo la Iringa mjini limeonekana kuwa nyuma kimaendeleo
kutokana na mbunge aliyekuwepo kuendekeza marumbano zaidi na
serikali na kushindwa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi wake kama
ilivyo kwa wabunge wengine wa CCM wanaomzunguka kama Isimani kwa Bw
wiliam Lukuvi na jimbo la Kalenga kwa Godfrey Mgimwa .
Alisema
kasi ya maendeleo katika majimbo jirani huwezi linganisha na
jimbo la Iringa mjini ambalo maendeleo yanayoonekana ni yale
aliyoacha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bi Monica Mbega na kipindi
cha miaka mitano ya Mchungaji Msigwa katika jimbo hilo zaidi ya
maandamano na lugha za kejeli kwa wananchi hakuna kilichofanyika
,hivyo ni lazima wananchi wa jimbo la Iringa mjini kutorudia kosa
kama la mwaka 2010
"
Tunajua wana CCM ndio tuliompeleka bungeni mchungaji Msigwa baada
ya chama ngazi ya juu kutosikiliza ma hitaji ya wananchi wa jimbo
hilo hasa wana CCM ambao walimpitisha katika kura za maoni na vikao
vya juu kukata jina lake ......ila kilichofanyika mwaka huu kwa
kurejesha jina la mshindi huyo Bw Mwakalebela ni sawa na kurejesha
ushindi kwa CCM"
Bw
Sanga alisema yeye akiwa katibu wa chama cha wazee mwenyekiti
wake alikuwa ni marehemu babake na Mwakalebela na kuwa siku zote
wazee wa jimbo la Iringa walikuwa kama wapweke kutokana na mbunge
huyo kuendeleza makundi na visasi .
Alisema
moja kati ya ahadi ambayo mchungaji Msigwa alipata kuwaahidi wazee
hao wakati wa kampeni ni pamoja na kutenga bajeti kupitia mfuko wa
jimbo kwa ajili ya kuwasaidia wazee na yatima ila hadi leo hajapata
kuonyesha hata senti moja iliyotengwa kwa ajili ya wazee hao jambo
ambalo linawafanya kujutia kura zao walizompatia mwaka 2010.
Sanga
alisema ilikuwa ni vema mbunge Msigwa angetembelea kujifunza kwa
mbunge wa mwaka mmoja wa jimbo la Kalenga kijana Mgimwa ambae ndani ya
mwaka mmoja alifanya mambo makubwa jimbo kwake tofauti na mbunge wa
miaka mitano ambae hana jipya la kuonyesha kwa muda wote aliokuwepo
madarakani .
Huku
Bi Salome Kalinga mkazi wa Kihesa Kilolo akidai kuwa ushindi wa
CCM unatokana na wana CCM wenyewe na ushindi wa Chadema kwa jimbo la
Iringa mjini utaletwa na wana CCM iwapo wataendeleza makundi kama
mwaka 2010 kwani kihalisia idadi ya wana CCM na wale wa vyama vya
upinzani jimbo la Iringa mjini bado CCM wapo wengi zaidi ila makundi
na visasi za kisiasa ndivyo vinavyopelekea chama kupoteza ushindi
wake .
Katibu
wa CCM kata ya Miyomboni Kitanzini Bw Rayson Shayo alisema kuwa
kata yake ambayo ndio kata iliyopo katikati ya mji wa Iringa hadi
sasa wanajutia kumchagua Msigwa kutokana na vurugu za mara kwa mara
ambazo chimbuko lake ni mbunge huyo ikiwemo vurugu ya machinga
kuruhusiwa na mbunge huyo kufanya kazi katikati ya barabara.
Share this article :