Home » » VURUGU KUBWA IRINGA, POLISI NA WANANCHI WAPAMBANA.

VURUGU KUBWA IRINGA, POLISI NA WANANCHI WAPAMBANA.

 
Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga barabara kwa kuwasha moto wa matairi ya gari.
Aidha taarifa kutoka kwenye eneo la tukio zinaendelea kueleza kuwa hadi sasa magari manne ya Polisi na Pikipiki moja vimechomwa moto, huku basi linalofahamika kwa jina la Nyagawa linalosafirisha abiria kutoka Njombe kuja Dar es Salaam likiwa limevinjwa vioo vyote.
Taarifa hizo zinadai kuwa tayari polisi wa kutuliza ghasia FFU wameshafika eneo la tukio na kufanikiwa kwa sehemu kutuliza ghasia hizo, na kwamba magari yanayokuja Dar es Salaam na mikoa mingine yameshaanza safari zake.
Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi
Chanzo Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa