Home » » KINANA ZIARANI IRINGA KWA SIKU SITA

KINANA ZIARANI IRINGA KWA SIKU SITA


2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu mara baada ya kuwasili mkoani Iringa kuanza ziara ya siku sita ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua uhai wa chama. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu na katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Hassan Mtenga.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA)1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozanana viongozi wa CCM mkoa wa Iringa Kulia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu na kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Hassan Mtenga. mara baada ya kuwasili mkoani Iringa asubuhi hii. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi mara baada ya kuwasili mkoani Iringa, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Hassan Mtenga. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Prof. Peter Msola mara baada ya kuwasili mkoani Iringa asubuhi hii tayari kwa kuendelea na ziara yake mkoani humo. 5Mbunge wa jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi kushoto akiwa na Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas na mbunge wa viti maalum Iringa Mh. Ritha Kabati. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali mara baada ya kuwasili mkoani Iringa leo asubuhi. 7Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman kinana ili awasalimie wananchi, kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Hassan Mtenga. 8Mmoja wa wahamasishaji akipiga kifaa cha Muziki cha kiasili mara baada ya katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuwasili mkoani Iringa. 11Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwasilimia wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mara baada ya kuwasili mkoani Iringa mkulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua jengo jipya la oisi ya CCM wilaya ya Iringa lililokarabatiwa na Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas pamoja na Mbunge wa jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi. 13Mbunge wa jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi, Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas na mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma wakimsikiliza Katinu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani ,wakati akitoa shukurani zake kwa waliojitolea kukarabati ofisi hiyo 14Katinu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimshukuru Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas ambaye amejitolea kukarabati ofisi ya CCM mkoa wa Iringa.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa