Home » » BACLAYS YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI

BACLAYS YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BENKI ya Barclays tawi la Iringa imetoa mafunzo ya utunzaji fedha kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Highlands ya mjini hapa  kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuhifadhi fedha sehemu salama.
Meneja wa Backlays tawi hilo, Shamsa Abdul Latiff, alisema hivi karibuni kuwa kila mtu anaweza kufikia ndoto ya mahitaji yake kama atakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Aliyataja mahitaji hayo kuwa ni kumudu gharama za elimu, ujenzi, ununuzi wa vyombo mbalimbali vya usafiri, vyakula na huduma nyingine muhimu kwa matumizi ya binadamu.

“Kwa kweli wanafunzi wanaweza kujiwekea akiba kutokana na kidogo wanachopewa na wazazi wao kwa ajili ya matumizi yenu ya kila siku muwapo shuleni, lakini pia mnaweza kusaidia kuwashauri wazazi na walezi wenu kujiepusha na matumizi yasio ya lazima ikiwemo matumizi ya pombe, ili mpate akiba,” alisema Latiff katika majadiliano yaliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo.

 Alitoa mfano kuwa katika kila sh. 1,000 anayopewa mwanafunzi kwa ajili ya matumizi yake shuleni, anaweza kujiwekea akiba ya hadi nusu ya kiasi hicho ambacho kwa mwaka kinaweza kuwa kikubwa.
Pamoja na hayo, alisema mafunzo hayo yanayotarajiwa kuwanufaisha wanafunzi wa shule nyingine mkoani hapa.
Awali, Ofisa Mikopo na Ufunguzi wa Akaunti wa benki hiyo, Charles Mwakameta, alizitaja njia nyingine za kutunza fedha kuwa ni kuficha sehemu mbalimbali majumbani kama kwenye mito na vitandani.
Zingine ni pamoja na kuhifadhi kwa kununua bidhaa mbalimbali kama vyakula kwa lengo la kuziuza pale unapohitaji fedha, kwa marafiki, kwenye makampuni ya simu, vikundi vya upatu na vyama vya kuweka na kukopa.
Kwa upande wao wanafunzi  walikiri matumizi ya pombe yanazifanya baadhi ya familia zao kukosa akiba.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa