Home » » ASILIMIA 95 YA WATOTO KUPEWA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA

ASILIMIA 95 YA WATOTO KUPEWA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa inatarajia kutoa chanjo ya surua na rubella kwa watoto 111,711 na dawa za matende na mabusha kwa watu wazima 264,076 katika kampeni inayoendelea nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo hiyo mkoani hapa, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Ignas Mlowe, alisema halmashauri hiyo imepewa lengo la kufikisha asilimia 95 ya utoaji wa chanjo hiyo na asilimia 100 kwa watu wazima katika ugawaji wa dawa za kinga ya matende na mabusha.
Alisema kampeni ya surua na rubella itatoa chanjo kwa watoto walio na miezi tisa mpaka chini ya miaka 15 na vidonge vya vitamini A kwa watoto wenye miezi sita mpaka 59.
Alisema kampeni hiyo iliyoanza rasmi Oktoba 18, mwaka huu imekumbwa na changamoto ya upungufu wa matone ya Vitamini A na kufutika kwa wino wa kuweka alama kidoleni pindi mtoto apatapo chanjo ya Surua na Rubella.
Alitaja changamoto nyingine ni uchache wa vituo vya kutolewa chanjo vilivyoanishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ingawa usambazaji wa vitendea kazi ikiwemo dawa za chanjo, matende na mabusha ukifanyika kwa asilimia 98 na usambazaji unaendelea kukamilisha asilimia 100.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Letecia Warioba, alisema uthibitisho wa kitaalam unaonyesha kuwa asilimia 85 ya watoto wanapata chanjo ya surua wakati wanapotimiza miezi tisa.
Alisema kampeni ya kitaifa ya surua na rubella ina lengo la kuwafikia watoto wote ambao hawakupa chanjo ya surua kabla na wale ambao hawakupata kinga kamilifu ili kuzuia ugonjwa huo na madhara yake
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa