Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANAWAKE wa Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba Wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa, wanaongoza kwa kujifungulia majumbani licha ya
elimu kutolewa kuhusu umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na
zahanati.
Akizungumza na Tanzania Daima, muuguzi wa zahanati ya Rungemba, Suzan
Mhngole, alisema pamoja na kujitahidi kutoa elimu kijiji hadi kijiji,
bado suala la kujifungulia katika zahanati, vituo vya afya na hospitali
kwa wananchi wa Kitelewasi ni changamoto.
Mhongole, alisema asilimia kubwa ya wanawake wanaobeba mimba katika
kijiji hicho ni wabishi wa kufuata maelekezo na ushauri wa wataalam
pindi wanapofika kliniki, na mwishoni hujifungulia majumbani mwao bila
kujali matatizo yanayoweza kujitokeza.
Alitaja sababu za kujifungulia majumbani ni kuwa, wengi wanapopewa
rufaa ya kwenda kujifungulia hospitali ya Wilaya, wamekuwa hawafanyi
hivyo na badala yake huenda kujifungulia majumbani.
“Tunapogundua kuwa mjamzito ana vidokezo vya hatari, tunamuandikia
rufaa ya kwenda katika hospitali kubwa lakini wengi tunaowaandikia
rufaa… wamekuwa hawaendi na badala yake wanaamua kwenda kujifungulia
majumbani mwao,” alisema.
Kata ya Rungemba ina vijiji vitatu, ambavyo vyenye zahanati ni
Rungemba na Itimbo huku Kitelewasi ikiwa haijakamilika kujengwa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment