Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WENYEJI wa Makete mkoani Njombe wanaoishi sehemu mbalimbali nchini,
wamekumbushwa wajibu waliyonao katika kuiendeleza Wilaya hiyo ili ikue
kiuchumi.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba
Tanzania (NHC), Nehemia Msechu, alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo
kwa lengo la kutembelea eneo litakalojengwa nyumba za bei nafuu kwa
wakazi wa Makete.
Alisema kabila la Wakinga ni wawekezaji wakubwa katika miji
mbalimbali, lakini inashangaza kuona wanasahau kuiendeleza Wilaya
wanayotoka na wangewekeza ingekuwa ni moja ya Wilaya yenye nguvu nchini
Tanzania.
“Inashangaza kuona Wilaya hii yenye hali ya hewa nzuri ikiwa katika
hali hii… ili hali tunashuhudia wazawa wa Wilaya hii wakifanya mambo
makubwa jijini Dar es Salaam hasa maeneo ya Kariakoo na sehemu
mbalimbali nchini,” alisema Msechu.
Alitoa wito kwa wazazi, uongozi wa Wilaya, viongozi wa dini na wadau
wengine wa maendeleo wilayani hapa, kuendelea kuwashawishi ili warudi
nyumbani na kuwekeza.
Taarifa kutoka jijini Dar es Salaam, zinaonyesha wakinga kwa kupitia
umoja wao, wamekuwa wakinunua nyumba za wenyeji na kujenga nyumba
nyingi za ghorofa kama vitega uchumi vyao.
Mbali na Dar es Salaam, Wakinga wanaonyesha uwezo wao kifedha katika
maeneo mikoa kama Morogoro, Arusha, Mwanza, Dodoma, Iringa na Mbeya.
Chanzo; Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment