Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKURUGENZI wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Kampuni ya Simu
Tigo, Jackson Kiswaga ametoa msaada wa pikipiki kwa jumuiya ya
Watumiaji Maji Kata ya Nzihi kwa lengo la kumaliza kero iliyokuwa
inawakabili ya usafiri ili kuwawezesha kutembelea mitambo mbalimbali
kwa urahisi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika hivi karibuni
katika ofisi za kata hiyo, Kiswaga aliahidi kuendelea kushirikiana na
wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Alisema apatapo fursa ya kukutana na watu wa ndani na nje ya nchi
wanaoweza kusaidia maendeleo ya watu wengine amekuwa akiyakumbuka
matatizo ya wananchi wa Iringa na kuomba msaada.
“Hakika katika kuleta maendeleo nitahakikisha nashirikiana na
wenzangu katika maendeleo yetu, sitaacha kutoa mchango wangu, nimefanya
hivyo muda mrefu uliopita, nafanya hivi sasa na nitaendelea kwa siku
zijazo, nimekutana na wadau kutoka Marekani, Ulaya na Afrika Kusini
kuna mambo yanakuja katika sekta ya afya na elimu na yatakapokuwa
tayari nitawaleta ,” alisema Kiswaga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Steven Mhapa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nzihi, alisema chombo
hicho cha usafiri kitaiwezesha jumuiya hiyo kusafiri eneo moja hadi
lingine kufuatilia maendeleo na changamoto zinazoukabili mradi huo wa
maji.
Naye Meneja wa Watumiaji Maji Kata hiyo, Hamza Chorobi, alisema mradi
huo wa maji una changamoto kama vile uchakavu wa miundombinu yake na
ongezeko la watumiaji wa huduma hiyo, hivyo unahitaji zaidi ya sh
milioni 300 kwa ajili ya ukarabati.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment