Home » » DALADALA ZAGOMA KWA SAA 8

DALADALA ZAGOMA KWA SAA 8

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
MABASI ya abiria ‘daladala’ yanayofanya safari zake mjini Iringa, jana yaligoma kwa saa 8 na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa na viunga vyake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva wa daladala hizo walisema sababu ya mgomo ni baadhi ya bajaji kuchukua abiria mithili ya daladala na kuwakosesha mapato.
Dereva Moses Job alisema bajaji zinafanyakazi za daladala huku mamlaka ya usafirishaji ikishindwa kuwachukulia hatua na kusababisha mgomo huo.
Mgomo huo ulimlazimu mwandishi wa habari hii kwenda ofisini kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Leopord Fungu na kushindwa kumwona baada ya kuambiwa yupo katika kikao na viongozi wa Kamati ya Usalama barabarani ya mkoa.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa