Home » » MPASUKO CCM IRINGA

MPASUKO CCM IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwenyekiti wa CCM Iringa, Jesca MsambatavanguJOTO la kuwania ubunge Iringa Mjini, katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani limeanza kuwagawa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa.
Mgawanyiko huo umekua zaidi baada ya kutangazwa kuwa sherehe za kumsimika kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa huo, zitafanyika Agosti 23 na Wilaya ya Iringa Mjini Agosti 29 mwaka huu.
Awali ilipangwa sherehe hizo zifanyike kwa siku moja lakini inadaiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa, Jesca Msambatavangu, ameingilia mchakato huo.
Inadaiwa anafanya hivyo kupunguza nguvu ya kujizolea umaarufu kamanda wa vijana wilaya ya Iringa Mjini atakayesimikwa Fredrick Mwakalebela anayetajwa kutaka kuwania ubunge kama inavyotajwa kwake.
Inaelezwa tishio la Msambatavangu ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ameshaanza maandalizi hayo na tishio kwake ni Mwakalebela.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Mwenyekiti huyo juu ya kuingilia mchakato wa sherehe hizo lakini hakuwa tayari kupokea wala kujibu ujumbe mfupi aliotumiwa.
Katibu wa CCM Iringa, Hassan Mtenga, alikana mkoa kuingiza mkono wake kwenye sherehe hizo kwakuwa kila kitu hufanywa na UVCCM.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Katibu wa UVCCM, mkoa Iringa Al Haidary Fumu, alisema wameamua kutenganisha sherehe hizo ili kutoa fursa ya kuzifanya kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa Kamanda wa UVCCM, Salim Abri Asas, akishaapishwa yeye ndiye atakuwa na jukumu la kumuapisha wa wilaya ambaye naye atawapisha wa kata.
“Mimi sijui kama kuna sarakasi za kuwania ubunge katika jambo letu, najua kufanya hivyo tutaongeza gharama lakini ni lazima tufunge mkaja,” alisema.
Naye Mwakalebela alisema kutenganishwa kwa sherehe hizo kutaongeza gharama kwakuwa maandalizi ya pamoja yalishafanyika.
“Haya mambo ya siasa yana vitu vingi, mimi naona wana CCM tuna kila sababu ya kuepuka kushughulikiana katika kuwania ubunge,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa